Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Konkoni: Bado nilikuwa na nafasi Yanga

Dar es Salaam. Hafiz Konkoni anayejiandaa kuondoka nchini kwenda kujiunga na timu ya Dogan Tûrk Birligi ya Cyprus kwa mkopo hadi mwisho wa msimu akitokea Yanga, amefichua kwamba, bado alikuwa na nafasi kwenye timu hiyo.

Konkoni aliyesajiliwa na Yanga msimu huu akitokea Bechem United ya Ghana kwa lengo la kuziba pengo lililoachwa na Fiston Mayele aliyepo kwa sasa Pyramids ya Misri, alishindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza, kabla ya uongozi kuamua kumtoa kwa mkopo Birligi kupitia dirisha dogo lililofungwa juzi Jumatatu.

Akizungumza na Mwananchi juzi usiku wakati akijiandaa na safari ya kuondoka nchini, Konkoni alisema anasikitika kuachana na Yanga katika kipindi hiki, kwani alikuwa anaiona nafasi yake kikosini kama angeendelea kuaminiwa, lakini kwa vile imeshatokea hana budi kukukubali.

Konkoni alisema Yanga inaundwa na wachezaji wenye viwango bora na wanaojituma uwanjani, ndio maana hata yeye alikuwa akipata ugumu kupenya kikosi cha kwanza na kwamba anaiona timu hiyo ikifika mbali zaidi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kulinganisha na watani wao wa jadi, Simba.

"Niwe muwazi kuwa, Yanga ina kikosi kizuri na wachezaji bora, naiona ikifika mbali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kuliko Simba kwani Yanga ina wachezaji wazuri sawa na Simba ila tofauti yao ni moja tu fitnesi. Yanga ina fitnesi ya hali ya juu kuliko Simba. Lakini mpira una maajabu yake wote nawatakia heri kwenye mashindano hayo," alisema Konkoni.

Mshambuliaji huyo aliongeza, anaondoka Yanga akiwa bado anaipenda na deni kubwa la kushindwa kutimiza malengo ya usajili ndani ya klabu hiyo.
"Haikuwa muda sahihi kwangu kuondoka Yanga, bado nina deni kubwa kwa mashabiki kwa vile sikupata nafasi ya kuitumikia vya kutosha, lakini sina namna kama ningepewa nafasi zaidi naamini ningeonyesha ubora wangu.