Kolabo ya AliKiba, Fally Ipupa yanukia

Friday October 08 2021
FALL KIBA PIC
By Nasra Abdallah

Mwanamuziki Fally Ipupa baada ya kufanya vizuri katika kibao cha 'Inama' alichoimba na msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz sasa ni zamu ya AliKiba.

Hayo yamebainishwa leo Ijumaa Oktoba 8, 2021 na Fally mwenyewe alipokutana na wandishi wa habari ambapo yupo nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya maonyesho yake mawili jijini Dar es Salaam na jijini Mwanza na kupewa jina la "Mahaba ya Rhumba'.

Inama ni wimbo uliotoka miaka miwil iliyopita na mpaka sasa umeshatazamwa mara milioni 97.

Mwanamuziki huyo alijikuta akizungumzia kolabo hiyo na AliKiba,baada ya kuulizwa namna alivyojisikia kibao cha Inama kikivyopokelewa na kama kupitia wimbo ule kuna msanii mwingine wa Tanzania ana mpango wakufanya nae kolabo au aliyemuomba kufanya naye kazi.

Akijibu hilo, Fally Ipupa amesema ni kweli wimbo umepokea vizuri na yote haya ni kutokana na uzuri wa wimbo wenyewe kuanzia biti mpaka mashairi.

Wakati kuhusu kufanya kazi na wasanii wengine wa Tanzania, amesema tayari kuna mpango wa kuachia ngoma na msanii AliKiba na tayari wapo katika hatua nzuri.

Advertisement

Kama haitoshi AliKiba ni mmoja waasanii watakaosidindikiza mwanamuziki huyo katika show yake ya kesho jijini Dar es Salaam.


Edward Lusala ambaye ni  Mratibu, wa kampuni ya Prime Time Promotions,waliomleta mwanamuziki huyo, amesema katika show hiyo mbali na AliKiba pia kutakuwa na wasanii wengine ambao ni 'suprise'.

Hata hivyo aliwashauri watu kujitokeza kwa wingi kwa kuwa ndio watakuwa wa kwanza kuonja utamu wa albamu ya sita ya msanii huyo kwa nchi za Afrika ambapo hii ni mara yake ya kwanza kuifanyia show.

Advertisement