Kocha Simba, Chico waibukia Mkwakwani

Sunday January 16 2022
Sajili PIC
By Charity James

ACHANA na ushindi waliousotea Yanga zaidi ya miaka saba dhidi ya Coastal Union katika Uwanja wa Mkwakwani ambapo leo wameondoa gundu kwa kutoa kipigo cha bao 2-0 huku wakifunga usajili wao kwa kutambulisha staa kutoka TP Mazembe, Chico Ushindi na kocha wa makipa Milton Nienov.

Kabla ya mchezo dhidi ya Coastal Union ambao wameibuka na ushindi wa bao 2-0, kabla ushindi na timu hiyo mara ya mwisho waliupata 2015 kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Ushindi na Milton wameonekana Tanga wakiwa wamevaa jezi za Yanga na muda mchache baadaye uongozi wa klabu hiyo ulitoa picha kwenye kurasa zao za Twitter na Instagram zikithibitisha usajili wao ndani ya timu.

Milton alishawahi kuwanoa makipa wa Simba kabla ya kutupiwa virago kwa madai kwamba hana vyeti vya kukidhi kukaa kwenye benchi la timu hiyo mapema mwaka jana.

Dirisha la usajili limefungwa usiku wa kuamkia leo na Yanga wamefanikiwa kusajili wachezaji sita na kocha mmoja wa makipa ambao wameingia kikosini humo kuongeza nguvu kuelekea kwenye harakati za kusaka taji la ligi na kombela FA baada ya kukosa Mapinduzi.

Nyota waliosajiliwa na Yanga dirisha hili la usajili ni Salum Abubakar 'Sure Boy', Denis Nkane, Crispin Ngushi, Abuutwalib Mshery, Ibrahim Abdallah 'Bacca' na Chico Ushindi.

Advertisement
Advertisement