Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Simba ailipua Yanga kuukosa ubingwa

KOCHA Msaidizi wa timu ya Simba, Masoud Djuma amefichua siri ya wapinzani wao Yanga kutumia wachezaji wengi wa kikosi cha pili kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons juzi Alhamisi uliochezwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Katika mchezo huo Yanga ilishangaza wadau wa soka nchini kutokana na kitendo cha kusafiri na wachezaji 13 pekee huku wengi kati yao wakiwa wachezaji ambao hawana nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kwenye timu hiyo jambo lililopelekea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Tanzania Prisons.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwandishi wa habari hii, Kocha Masoud Djuma alisema anaamini sababu za Yanga kuwenda Mbeya na wachezaji pungufu ilitokana na ushauri aliompatia Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa siku walipoifunga timu hiyo bao 1-0 uwanja wa Taifa.
“Niwe muwazi bila kuficha kuwa ushauri wangu nilioutoa kwa kocha msaidizi wa Yanga, ndio ambao nimeuona ukifanyiwa kazi na benchi la ufundi la timu yao ambapo siku tuliyowafunga bao 1-0 Uwanja wa Taifa baada ya mechi nilimwambia ukweli nguvu zao zote waelekeze Kombe la Shirikisho wana nafasi ya kufanya vizuri na sio lLigi Kuu kwa sababu ni msimu wa Simba,” alisema Djuma.
Djuma ambaye anasaidiana na Mfaransa, Pierre Lechantre aliongeza kuwa yupo tofauti na watu wanaoponda kitendo cha Yanga kutumia wachezaji wa akiba na kuwaacha wachezaji muhimu jijini Dar es Salaam. Badala yake wapo sahihi zaidi kuwekeza nguvu zao kwenye mechi ijayo ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda itakayopigwa Mei 16 uwanja wa Taifa.
“Mimi nawashangaa watu wanaoponda na kushangaa kitendo walichofanya Yanga kutumia wachezaji wasio na nafasi kikosi cha kwanza, wako sahihi sana ndivyo walipaswa kufanya kwa sababu wanatakiwa kukusanya nguvu zaidi ya kupambania ushindi kwenye mechi za kundi lao la Shirikisho Afrika na ndio sehemu pekee wanaweza kufanya maajabu tofauti na ligi kuu” alisisitiza Mrundi huyo.
Kichapo walichokipata Yanga kutoka kwa Tanzania Prisons jana jijini Mbeya ndicho kilichowavua ubingwa wa Ligi Kuu ambao wameushikilia kwa misimu mitatu mfululizo tangu walipouchukua mikononi mwa Azam ambapo Yanga licha ya kuwa na mechi 5 mkononi hazitosaidia kuifikia Simba yenye alama 65 juu ya msimamo wakati Yanga wanazo alama 48.