Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Oscar Tabarez aweka historia Kombe la Dunia Russia

Muktasari:

  • Tabarez alizaliwa tarehe 3 Machi 1947. Amewahi kuitumikia timu hiyo nafasi ya beki na sasa ameiongoza kwa mara nyingine hadi hatua ya robo fainali, huku timu hiyo ikipokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Ufaransa katika mchezo wake wa kwanza hatua hiyo.

Kocha wa Uruguay, Oscar Tabarez ameandika historia kwenye fainali za Kombe la Dunia Urusi kuwa kocha mzee kuongoza timu ya Taifa kwenye mashindano hayo.

Tabarez alizaliwa tarehe 3 Machi 1947. Amewahi kuitumikia timu hiyo nafasi ya beki na sasa ameiongoza kwa mara nyingine hadi hatua ya robo fainali, huku timu hiyo ikipokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Ufaransa katika mchezo wake wa kwanza hatua hiyo.

Kocha huyo ameiongoza timu hiyo kwenye Kombe la Dunia mara tatu, huku akizifundisha timu mbalimbali za taifa nchini humo.

Itakumbukwa aliiongoza Uruguay kwenye Kombe la Dunia mwaka 1988-1990. Pia aliiongoza timu hiyo mwaka 2006 na amekabidhiwa mikoba kwa mara nyingine mwaka huu kuinoa fainali za Kombe la Dunia Russia 2018.

Ushindi wa Ufaransa wa mabao 2-0 umewarudisha vijana wa Tabarez nyumbani huku wababe wa soka Ufaransa wakiwa timu ya kwanza kutangulia hatua ya nusu fainali.