Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Msauz achukua mikoba ya Pedro Yanga

Muktasari:

  • Manqoba ambaye ni kocha wa zamani wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha Yanga.

Yanga imemtambulisha kocha Manqoba Mngqithi kuwa kocha wao mpya akichukua nafasi ya Pedro Goncalves.

Manqoba ambaye ni kocha wa zamani wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha Yanga.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema kocha huyo ataanza kazi haraka ya kuandaa kikosi hicho tayari kwa msimu ujao.

Kocha huyo mwenye mafanikio makubwa nchini Afrika Kusini anatua Yanga ikitaka aipe mafanikio kwenye soka la Afrika.

Manqoba (56) anatua Yanga akitokea Golden Arrows ya Afrika Kusini, iliyomaliza nafasi ya sita msimu uliopita wa Ligi ya nchini humo.

Bado Yanga haijaweka wazi kuwa kocha huyo atatua nchini lini kuanza kazi hapa nchini kukiandaa kikosi cha Mabingwa hao.

Awali Yanga ilihusishwa na kocha Fadlu Davids lakini Mwanaspoti linafahamu kwamba pande hizo mbili zilishindwana mezani wakati wa makubaliano.