Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Milambo awaita mashabiki Uwanja wa Taifa

SUDAN ilipoteza mechi ya kwanza kwa kufungwa mabao 3-1 na Rwanda kitu kilichomfanya kocha wa timu, Zdravko Logarusic aliyewahi kuinoa Simba kutamka timu yoyote itakayokuja mbele yake ni kipigo tu ikiwamo Tanzania iliyopo nayo kundi moja.

Wanyarwanda hao jana Jumatatu walitarajiwa kuvaana na majirani zao wa Burundi waliolala 2-1 kwa Tanzania, lakini mkwara waliochimbia umeshtua Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Milambo ambaye ameamua kuwaita mashabiki Uwanja wa Taifa.

“Kufungwa mechi ya kwanza hakumaanishi nimekata tamaa, nitahakikisha mchezo utakaofuata ninashinda nitaenda kuwajenga wachezaji wangu hasa kufanya marekebisho mapungufu niliyoyaona,” alisema Kocha Logarusic, lakini Milambo hakutaka kubaki nyuma na kusema hawapoi kazi ni moja tu kugawa vipigo.

“Niwaombe Watanzania wajitokeze kwa wingi tutakapocheza dhidi ya Sudan Alhamisi hii, naamini vijana wangu hawatawaangusha.

“Vijana wana morali ya kuifanyia kitu nchi yao kupitia michuano hii, kiufundi wapo vizuri na wamejifua, hatuwapuuzi Sudan ndio maana mechi hii tunaichukulia kama fainali, tutacheza kwa nidhamu ya juu,” alisema Milambo.