Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Kim atema 10 Kilimanjaro Warriors

Dar es Salaam. Wachezaji kumi (10) watatemwa katika kundi la nyota 35 wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya vijana wenye umri usiozidi miaka 23 'Kilimanjaro Warriors' kinachojiandaa na mashindano ya kuwania kufuzu michezo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan 2020.

 

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Oscar Milambo alisema panga hilo kwa wachezaji wanaounda kikosi hicho, litapita baada ya kambi ya mazoezi ya siku 10 inayoendelea katika uwanja wa Karume jijini iliyoanza Jumatatu ya wiki iliyopita.

 

Milambo alisema wameamua kupitisha mchujo huo ili benchi la ufundi libakie na nyota 25 na pia kutoa nafasi kwa vijana wengine watakaoonyesha kiwango kizuri kwenye klabu zao katika mechi zitakazochezwa hivi karibuni, ili wapate kikosi bora kitakachoiletea mafanikio timu hiyo.

 

"Hawa wachezaji wamepatikana kutokana na ripoti tuliyoletewa na makocha wa timu zao pamoja na uskauti tulioufanya katika mashindano ya vikosi vya vijana wenye umri usiozidi miaka 20 kwa klabu zinazoshiriki ligi pamoja na mechi mbalimbali za Ligi Kuu.

 

Ndio maana tukaamua kuendesha kambi hii ya siku kumi ili kujiridhisha kuhusu kiwango chao na tutawapunguza wachezaji 10 ambao kiwango chao kitashindwa kutushawishi kuendelea nao kwa ajili ya mashindano yaliyo mbele yetu. Hata hivyo nafasi bado iko wazi kwa wachezaji wengine wenye umri huo kuingia kikosini iwapo watafanya vizuri katika mechi za ligi," alisema Milambo.