Kocha JKU aichimba mkwara Azam

Muktasari:
- Mtuli alisema wanatambua wanatarajia kukutana na mabingwa watetezi wa kombe hilo kesho, lakini hawana wasiwasi wowote zaidi wanafanya maandalizi ya nguvu ili kuonyesha ubora wao na kutimiza malengo.
Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa JKU ya Zanzibar, Ali Suleiman Mtuli amesema anakikosi bora hivyo hana wasiwasi na timu yoyote inayoshiriki Kombe la Kagame na kuwaambia Azam wasitegemee mteremko katika mchezo dhidi yao.
Mtuli alisema wanatambua wanatarajia kukutana na mabingwa watetezi wa kombe hilo kesho, lakini hawana wasiwasi wowote zaidi wanafanya maandalizi ya nguvu ili kuonyesha ubora wao na kutimiza malengo.
"Tumecheza michezo miwili tumeshinda mmoja na kutoka sare mchezo mmoja tunaamini ata timu tulizocheza nazo ni bora hivyo tutaendeleza changamoto ya ushindani pia katika mchezo wetu na Azam FC kubwa tunawaomba mashabiki kutufanyia dua kuelekea mchezo huo ili tuweze kushinda."
Aliongeza hawana majeruhi yeyote katika kikosi chao kila mchezaji yupo katika hari ya mchezo wanategemea ushindani zaidi katika mchezo wao na Azam na kuweka wazi kuwa wanaamini wataibuka na ushindi katika mchezo huo.