Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Ceasiaa Queens alia na waamuzi

CHOBANKA Pict

Muktasari:

  • Ceasiaa iko nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi baada ya mechi 13, ikishinda tano, sare moja na kupoteza saba na imekusanya pointi 16.

KOCHA wa Ceasiaa Queens, Ezekiel Chobanka amesema kuna haja waamuzi kuchezesha vyema mechi na kuacha kupendelea timu moja hasa kubwa.

Ceasiaa iko nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi baada ya mechi 13, ikishinda tano, sare moja na kupoteza saba na imekusanya pointi 16.

"Sisi tumekuwa tukionewa sana mechi ya juzi na JKT mwamuzi anakataa mabao mawili tuliyofunga, kila tukienda kushambulia anasema tumeotea nikawaambia wachezaji wangu wacheze tu hakuna namna zaidi ya hilo," alisema Chobanka.

Aliongeza "Pamoja na changamoto hiyo, nafikiri tunaanza kujiandaa mapema na mechi sita zilizobaki, kwetu ni ngumu sana hasa ya Yanga ambayo tutakuwa ugenini, lakini tumeanza maandalizi mapema kuhakikisha tunaonyesha mchezo mzuri wenye ushindani."