Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KMC yamtimua Humoud kisa kutongoza mchumba wa mwenzake

Muktasari:

Humoud ameachwa na KMC ikiwa na mchakato wa wanasheria kuangalia kwa namna gani watambana mchezaji huyo ambaye hajamaliza miezi hata minne toka aliposaini mkataba mpya Julai mosi mwaka huu.

Dar es Salaam. Kiungo Abdulhalim Humoud 'Gaucho' (31) amefyekelewa mbali katika kikosi cha KMC kwa madai ya kumtongoza mchumba wa mchezaji mwenzake.

Humoud ambaye aliipandisha daraja timu hiyo ya manispaa ya Kinondoni ndiye aliyeomba kuachwa katika kikosi hicho kufuatia kuhisi kutokuwa katika mipango kocha mkuu, Etienne Ndayiragije.

Akizungumzia kuhusu kuachwa kwa Humoud, Katibu msaidizi wa KMC, Walter Harrison alisema hawakuwa na chaguo lingine zaidi ya kuachana na kiungo huyo kutokana na matendo yake ya utovu wa nidhamu.

"Tukio la kwanza kwa Humoud lilijitokeza katika mchezo dhidi ya Coastal Union ambapo hakuanza katika kikosi cha kwanza, kocha alipohitaji kumtumia alisema ameacha vifaa vyake Dar.

"Kama viongozi tulikaa naye chini na kulimaliza, lakini siku chache baadaye yakatokea mengine, Humoud alichukua simu ya mwenzake ambaye anakaa naye chumba kimoja na kuchukua namba ya mchumba wake na kuanza kumtongoza," alisema Harrison.

Katibu huyo msaidizi alisema tabia hiyo ilimchefua kocha na hata viongozi ambao kwa pamoja walikaa chini na mchezaji huyo ambaye aliamua kuomba radhi, lakini muda mchache baadaye aliandika barua ya kuombwa kuachwa.

Harrison alisema kama viongozi ilibidi wakae chini kwa kumshirikisha kocha na kuamua kuachana na mchezaji huyo aliyewahi kutamba akiwa na Simba, Azam.

Hata hivyo; kabla ya kuamua kuachana naye Harrison alisema waliwahi kupokea malalamiko ya Humoud kutoka mwa mchezaji wa timu nyingine akidai kiungo huyo amekuwa akimsumbua mke wake mara kwa mara.