Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Klopp macho kodo kwa staa Timo Werner

Muktasari:

Kwa mujibu wa Sport Bild, Klopp anataka kukutana ana kwa ana na Werner azingumze naye binafsi kuona kama kuna kitu chochote ataweza kumshawishi na kukubali kwenda kukipiga huko Anfield.

LIVERPOOL, ENGLAND .KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp anataka kukutana na straika Timo Werner kwanza kabla ya kukamilisha mchakato wa kunasa huduma ya mkali huyo wa RB Leipzig.

Klopp kwa muda mrefu sana amekuwa akivutiwa na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, ambaye anataka kupiga hatua ya mbele kwenye soka lake ikiwamo kwenda kujiunga na timu itakayocheza kwa ubabe mkubwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Straika Werner anaonekana kuwa kwenye mipango ya kocha huyo wa Liverpool kwa sababu anafahamu wazi atapatikana kwa gharama ndogo kuliko washambuliaji wengine kama Jadon Sancho, Kylian Mbappe.

Kwa mujibu wa Sport Bild, Klopp anataka kukutana ana kwa ana na Werner azingumze naye binafsi kuona kama kuna kitu chochote ataweza kumshawishi na kukubali kwenda kukipiga huko Anfield.

Kinachoelezwa ni mkwamba wawili hao, Klopp na Werner wangekuwa wameshakutana hadi kufika sasa kama maambukizi ya virusi vya corona yasingekuwa yameshika kasi zaidi.

Bayern Munich nao wanamhitaji

Werner alizungumzia kuhusishwa na Liverpool akiisifu baada ya kuisaidia timu yake kuichapa Tottenham Hotspur kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.