Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo mshambuliaji Raja Casablanca atua Azam

Azam FC imeanza kushusha vifaa kwa ajili ya msimu ujao baada ya kupitisha fagio la wachezaji ambao hawataendelea nao.

Leo Azam imeanza kwa kutambulisha mshambuliaji aliyenunuliwa kutoka klabu ya Raja Casablanca, Djirril Sillah.

Kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii wameandika;  "Tunayofuraha kuwataarifu kuwa tumefikia makubaliano na klabu ya Raja Casablanca, ya kumnunua kiungo wao mshambuliaji, Sillah,"

Nyota huyo wa Gambia, anatarajia kutua nchini muda wowote kuanzia sasa kumalizia taratibu za mwisho za usajili.

Msimu uliopita kwenye Ligi Kuu ya Morocco, Sillah alifanikiwa kufunga jumla ya mabao saba na kutoa pasi za mwisho nne, wakati akiwa kwa mkopo JS Soualem.