Kiungo Mnigeria aigawa Simba

SOKA lililopigwa na kiungo Mnigeria, Etop Udoh, umewagawa mabosi wa klabu hiyo baadhi wakitaka asajiliwe na wengine wakitaka maamuzi ya mwisho yawe ya kocha aliyenaye kwa sasa kambini akimfanyia majaribio.
Udoh aliyewahi kukipiga nchini Tunisia na Armenia na Saudi Arabia, ni kati ya wachezaji watatu waliojiunga na Simba ili kujaribiwa kabla ya kusajiliwa akiwamo Msudan Shiboub Sharraf na Cheick Moukoro kutoka Ivory Coast.
Inaelezwa Shiboub na Moukoro wameshindwa kumvutia kocha Pablo Franco, lakini Udoh aliyeingia kwa dakika zisizozidi 15 katika mechi dhidi ya Mlandege kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi amewavutia Wanasimba kwa soka lake.
Inaelezwa miongoni mwa vigogo waliovutiwa na kiwango cha Mnigeria huyo ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’, Mjumbe wa bodi, Mlamu Nghambi na Crescentius Magori, lakini wanashindwa kuamua lolote kwa sasa wakimsikilizia Kocha Pablo.
Uwezo wa Kucheza hasa anapokuwa na mpira kwa kuanzisha mashambulizi kwa kupiga pasi ndefu na fupi zinazofika kwa walengo, akiwa pia anakaba timu inaposhambulia imewadatisha mabosi hao wa kutamani asainishwe, lakini usajili mzima kwa sasa ameachiwa Pablo.
Inadaiwa kwa sasa Pablo amekuwa mzito kufanya maamuzi juu ya Udho kwa vile anakunwa na soka la Jonas Mkude anayevutiwa na soka lake, huku pia akiwa na jembe jingine katiak eneo hilo la kiungo cha ukabaji, yaani Taddeo Lwanga mbali na Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute.
Udoh alipotafutwa na Mwanaspoti, alisema; “Juu ya majaribio naamini nitafanya vizuri, nakiamini kiwango changu, kama nikishindwa kubaki hapa, basi labda iwe kwa kitu kingine.”