Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Mbrazil ajipeleka Chelsea

Muktasari:

Oscar alitimkia Beijing kucheza katika klabu ya Shanghai SIPG ya Ligi Kuu China iliyomnunua kwa Sh52 Paundi.

Rio de Janeiro, Brazil. Kiungo wa zamani wa Chelsea, Oscar ameibuka na kudai anataka kurejea makao makuu Stamford Bridge.

Oscar alitimkia Beijing kucheza katika klabu ya Shanghai SIPG ya Ligi Kuu China iliyomnunua kwa Sh52 Paundi.

Pia kiungo huyo mshambuliaji alikuwa akilipwa mshahara mnono wa Sh400,000 Paundi kwa wiki akiwa ni mmoja wa wachezaji wanaolipwa vizuri nchini humo.

Oscar alisema amekumbuka Ligi Kuu England na anataka kucheza Chelsea." Ndio nataka kurudi bado ni kijana mdogo wa miaka 26, kama itachukua miaka miwili au mitatu nitakuwa na furaha kurejea Chelsea," alisema Oscar.

Mbrazil huyo alisema aliamua kuondoka Chelsea baada ya kocha Antonio Conte kubadili mfumo wa uchezaji uliomnyima nafasi ya kucheza.