Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Mamelodi amjibu Mayele

Baada ya ushindi wa bao 1-0 wa Mamelodi Sunsowns dhidi ya  Pyramids FC iliyokuwa nyumbani kwenye Uwanja wa June 30, Cairo, Misri,  mchezo wa nne wa kundi A,  Ligi ya Mabingwa Afrika, kiungo wa timu hiyo, Teboho Mokoena   amemjibu Fiston Mayele  kwa kile alichoandika  kwenye akaunti yake ya Instagram. Mayele baada ya kushindwa kusafiri na timu yake ya Pyramids FC kwenda Afrika Kusini kwenye mchezo wa kwanza, aliandika; "Sawa ulikataa kunipa visa ukiamini utatupiga subutu, pointi 1 muhimu tukutane sasa Cairo."

Sasa baada ya matokeo ya ushindi wa Mamelodi, Mokoena amejibu kwenye posti hiyo iliyoandikwa wiki moja zilizopita,

“Ulikuwa unasema?”, ikiwa ni kijembe kwa nyota huyo aliyewahi kutamba na Yanga akiifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika kundi hilo, Memolodi inaongoza na pointi saba sawa na TP Mazembe huku Pyramids ikiwa nafasi ya tatu na pointi  nne sawa na Nouadhibou.