Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kitonga cha bidhaa mtandaoni chazidi kuwafurahisha watanzania

Kimewaka Pict

Muktasari:

  • Mambo hayo yanaletwa na mnada wa Piku Africa,  na miongoni mwa washindi hao ni Sara Kyando (23), mkazi wa Kinondoni na mfanyakazi wa kampuni ya moja inayojishughulisha na masuala ya elimu na amejishindia simu Janja aina ya Samsung A06 yenye thamani ya Sh250,000.

UNAKAA kinyonge na una simu janja? Wenzako wanazidi kufurahia maisha kwa kujinyakulia zawadi mbalimbali mtandaoni, huku watatu jijini Dar es Salaam wakiondoka na bidhaa zenye thamani ya Sh3 milioni.

Mambo hayo yanaletwa na mnada wa Piku Africa,  na miongoni mwa washindi hao ni Sara Kyando (23), mkazi wa Kinondoni na mfanyakazi wa kampuni ya moja inayojishughulisha na masuala ya elimu na amejishindia simu Janja aina ya Samsung A06 yenye thamani ya Sh250,000.

Akizungumza na waandishi wa habari, Sara amesema aligundua kuhusu mnada huo katika mtandao wa Instagram na baada ya kuona washindi wengine, alihamasika kushiriki.

“Nilijaribu kucheza na kushinda. Nawashauri vijana wenzangu watumie vizuri mitandao ya kijamii kwa kushiriki katika minada kama hii, kwani inaweza kuwasaidia kupata bidhaa bora na kwa gharama nafuu,” amesema Sara kwa furaha.

Mshindi mwingine ni Gloria Emil (28), mkazi wa Tegeta, ambaye amejinyakulia na yeye simu janja aina ya Samsung A06, amesema amefurahia zawadi hiyo kwa kuwa simu yake ya awali ilikuwa imeharibika.

“Kupitia simu hii mpyaniliyopewa nitakuwa na mawasiliano bora zaidi na ndugu zangu pamoja na wateja wangu. Nawashukuru mnada huu kwa urahisi huu, kwani wamenisaidia katika kufanikisha biashara zangu,” amesema Gloria.

Kwa upande wake, Obeid Joshua (20) mkazi wa Mbezi, ambaye amejinyakulia televisheni aina ya LG pamoja na router ya Airtel yenye bando la mwaka mzima, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 2.4, amesema mnada huu ni wa kipekee na unaowavutia watu wengi hasa vijana.

Obeid amesema aliufahamu mnada huu katika mitandao ya kijamii baada ya kuona tangazo la mshindi wa bodaboda, jambo lililomhamasisha kujaribu bahati yake na hatimaye amejinyakulia bidhaa nzuri na yenye ubora.

“Najisikia furaha sana kushinda bidhaa hizi. mnada huu ni wa kweli kabisa, siyo janja janja. Nawashauri vijana wenzangu wasisite kushiriki. Hata kama hukushinda mara ya kwanza, endelea kujaribu kwa sababu bidhaa ni nyingi na kila siku kuna nafasi mpya ya kushinda,” amesema.

Kwa upande wake, balozi wa mnada huo, Saphiness Rabieth amesema jukwaa hilo limejipanga vizuri kuhakikisha washiriki wote wanapata bidhaa za kisasa na zenye bora wa hali ya juu.

“Tunatoa zawadi nyingi kila siku, ikiwemo simu janja aina ya Samsung A06 kila baada ya siku tatu. Wateja wanachotakiwa kufanya ni kupakua App ya Piku kwenye Play Store kwa watumiaji wa Android au App Store kwa wenye iPhone. Tiketi za mnada zetu zinapatikana kuanzia Sh. 1,000 hadi 100,000,” amesema Rabieth.

Kwa jumla, washiriki wa mnada huo wanaendelea kuthibitisha jukwaa hili ni la kweli, lenye uwazi na fursa halisi za kujishindia bidhaa bora kwa dau dogo na la kipekee.
Mwishooo