Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Prisons, Polisi Tanzania katika mvutano mpya Ligi Kuu

VITA Pict

Muktasari:

  • Timu hizo zinakutana leo Alhamisi Julai 16, 2026 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ikiwa kila upande una hesabu zake za kusaka heshima ya kucheza Ligi Kuu, ambapo Polisi Tanzania inajivunia mtaji wa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza iliyopigwa Julai 12, 2026 mjini Moshi.

KAZI ipo. Ndivyo unavyoweza kusema kuelezea presha ya mchezo wa kukamilisha mtoano ‘play off’ kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Polisi Tanzania utakaoamua hatma ya timu mojawapo kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

Timu hizo zinakutana leo Alhamisi Julai 16, 2026 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ikiwa kila upande una hesabu zake za kusaka heshima ya kucheza Ligi Kuu, ambapo Polisi Tanzania inajivunia mtaji wa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza iliyopigwa Julai 12, 2026 mjini Moshi.

Hata hivyo, licha ya kuwa na faida ya mabao hayo, itapaswa kuingia uwanjani kwa nidhamu dhidi ya wapinzani ikisaka japo sare ili kujihakikishia kupanda daraja, vinginevyo maajabu ya mpira huenda yakawakuta.

POLI 01

Msimu wa 2025-2026, Polisi Tanzania ilishiriki Championship ilipomaliza nafasi ya tatu kwa pointi 66, ambapo inasaka rekodi ya kurejea Ligi Kuu kupitia play off kama zilivyowahi kufanya Ihefu iliyoitoa Mbao FC na Mashujaa iliyofanya hivyo kwa Mbeya City.

Timu hiyo ya Jeshi la Polisi nchini, inasaka heshima ya kurejea Ligi Kuu kupitia play off baada ya kudumu Championship misimu mitatu tangu iliposhuka daraja msimu wa 2022-2023.

Prisons iliyomaliza Ligi Kuu nafasi ya 13 kwa pointi 32, ndio yenye kibarua kizito cha kufanya maajabu ya ‘Comeback’ kurejesha mabao manne na kusaka la ushindi ili kubaki salama Ligi Kuu.

POLI 02

Prisons  inacheza play off kwa mara ya pili kwenye historia tangu walipofanya hivyo msimu wa 2021-2022 walipokutana na JKT Tanzania na kushinda kwa jumla ya mabao 2-1.

Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Shadrack Nsajigwa, amesema licha ya kupoteza mchezo uliopita lakini bado wanayo matumaini ya kufanya vizuri na kufikia malengo yao huku akikiri kazi haitakuwa nyepesi.

“Mpira lolote linawezekana, kimsingi ni kuendelea kupambana kwa dakika 90 zilizobaki, vijana wako tayari kupigania heshima ya timu kuhakikisha tunabaki salama, tunajua ugumu uliopo ila lolote linawezekana,”  amesema Nsajigwa.

Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Mbwana Makata, amesema ushindi walioupata licha ya kuwapa matumaini, lakini hawatadharau wapinzani kwakuwa wanayo malengo msimu huu kuhakikisha wanaandika rekodi.

“Pamoja na matokeo ya mchezo wa kwanza ila lazima tuwe na nidhamu ya mpira kwa wapinzani, bado hatujamaliza safari na hatuwezi kubweteka kwa ushindi wa awali, lazima tupambane.”