Kisinda aanza na Ruvu Shooting

WINGA mpya wa Yanga, Tuisila Kisinda aliyesajiliwa na timu hiyo dakika za mwisho kabla ya dirisha la usajili wa Ligi Kuu Bara kufungwa ameanza katika cha kwanza dhidi ya Ruvu Shooting.
Saa 12:15 jioni mchezo utaanza kati ya Yanga iliyokuwa ugenini itacheza dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kwenye kikosi cha Yanga, Kisinda aliyekosa mechi za kimashindano kutokana na kushindwa kupata kibali ameanza baada ya suala lake hilo kukamilika.
Tuisila aliyesajiliwa na Yanga akitokea RS Barkene ya Morocco ameanza kwenye eneo ushambuliaji akitokea pembeni.
Kikosi cha Yanga, kimeanza na mabeki wanne, Djigui Diarra, Djuma Shabani, Joyce Lomalisa, nahodha Bakari Mwamnyeto na Dickson Job.
Katika eneo la kiungo wameanza watatu Yanick Bangala, Salumu Abubakar na juu yao akicheza Feisal Salum.
Eneo la kushambulia wapo, Farid Mussa, kinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga, Fiston Mayele aliyeweka kambani matatu hadi sasa kwenye ligi na Kisinda.
Kuingia kwa Kisinda kwenye kikosi cha kwanza amechukua nafasi ya Aziz Ki au Benard Morrison ambao wamekosekana katika kikosi cha kwanza kwa sababu mbalimbali.
Morrison anatumikia adhabu, Ki bado hajarejea nchini kutokana kukwama huko Morocco alipokuwa na kikosi cha timu Bokinafaso.
Ki akiwa nchi Morocco inaelezwa alikutwa na virusi vya uviko 19, ndio maana amechelewa kurejea nchini kujiunga na timu.
Wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza na wamekosekana katika mchezo huu, Khalid Aucho ambaye ni majeruhi ila yupo kwenye benchi la akiba kama ilivyo kwa beki, Kibwana Shomary.
Katika benchi la akiba wapo, Aboutwalib Mshery, Kibwana, Ibrahim Bacca, Zawadi Mauya, Khalid Aucho, Denis Nkane, Heritier Makambo, Dickson Ambundo na Clement Mzize.