Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Kocha Stars, TFF yapewa mchongo

Muktasari:

  • Tangu aondoke Honour Janza (Desemba mwaka jana) ambaye ameenda kuwa mkurugenzi wa ufundi katika klabu ya Zesco ya Zambia, Stars ilikuwa ipo chini ya makocha wasaidizi Mecky Maxime na kocha wa makipa Juma Kaseja.

KITENDO cha Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kukaa kimya hadi sasa juu ya kocha mkuu wa timu ya Taifa Tanzania, kimewaibua wadau mbalimbali wa soka na kuhoji namna wachezaji watakaounda timu watakavyopatikana.

Tangu aondoke Honour Janza (Desemba mwaka jana) ambaye ameenda kuwa mkurugenzi wa ufundi katika klabu ya Zesco ya Zambia, Stars ilikuwa ipo chini ya makocha wasaidizi Mecky Maxime na kocha wa makipa Juma Kaseja.

Mshambuliaji wa zamani Yanga, Hery Morris alisema makocha wengi wanaokuja bado wameshindwa kufanya vitu vikubwa katika timu ya Taifa hivyo kama hadi sasa hajapatikana kocha ni bora liundwe jopo la makocha wazawa na kuchagua wachezaji kwa ajili ya mechi za kimataifa.

“Kama kuna shida ya kupata kocha mkuu ni bora timu kwanza itafute wachezaji kwa kuundwa jopo la wazawa kama Mayanga (Salum), Mgunda (Juma), Mkwasa (Charles) na wengineo halafu wakae na kuchagua wachezaji kwa sababu wao wanawaona mara kwa mara.

“Hii wafanye kwa sababu hawajapata bado kocha mkuu na siku zinazidi kwenda na timu inatakiwa kuingia kambini.” Upande wa mshambuliaji wa zamani wa Simba, Bakari Kigodeko alisema kwa kifupi;”TFF inajielewa na hata kama kocha mkuu hayupo si kuna wasaidizi wake kwa hiyo wanaweza kutangaza majina na timu ikacheza.”

Mchezaji wa zamani Simba, Yanga na timu ya Taifa Tanzania, Zamoyoni Mogela alisema “Unajua timu ya Taifa, kocha mkuu anaweza kufuatilia wachezaji nchi mbalimbali lakini kwa kocha msaidizi sina hakika sana, kuna tatizo na siasa imeingia tayari kwenye mpira wetu wa miguu;

“Ukija kuangalia mara nyingi huwa tunachukua wachezaji Simba na Yanga, je huko wazawa wanafanya vizuri kwa kiwango kikubwa kiasi cha kuitwa katika timu ya Taifa, hilo sina hakika.”

Alipotafutwa Mkurugenzi wa Ufundi TFF, Oscar Milambo simu yake iliita bila kupokelewa.

Stars inashika nafasi ya tatu kwenye kundi F ya kutafuta nafasi ya kufuzu AFCON ikiwa na pointi moja katika mechi mbili ilizocheza huku anayeongoza ni Algeria yenye pointi sita.

Stars itakuwa na mchezo wa kufuzu Fainali za kimataifa Afrika (AFCON), dhidi ya Uganda Machi 24 nchini Uganda na marudiano ni Machi 28, Uwanja wa Mkapa, Dar.

Baada ya mchezo huo, Stars itacheza na Niger Kwa Mkapa (Juni 12) na itasafiri kwenda Algeria kucheza nao Septemba 4.