Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipigo chaishtua Srelio, yafuata mastaa DR Congo

Muktasari:

  • Katika michezo ya awali ya mashindano hayo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Donbosco, Upanga, timu hiyo ilifungwa na Mchenga Star kwa pointi 82-70, Dar City 105-32 kisha  ikaifunga Chui kwa pointi 55-52 huku mchezo wa nne ikifungwa na Pazi kwa pointi 81-73.

BAADA ya Srelio kufungwa na Pazi kwa pointi 81-73 katika mchezo wa Ligi ya Kikapu Dar es Salaam (BDL), kocha wa timu hiyo, Miyasi Nyamoko amesema wameamua kuwaita nyota wawili kutoka DR Congo ili waje kuokoa jahazi.

Katika michezo ya awali ya mashindano hayo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Donbosco, Upanga, timu hiyo ilifungwa na Mchenga Star kwa pointi 82-70, Dar City 105-32 kisha  ikaifunga Chui kwa pointi 55-52 huku mchezo wa nne ikifungwa na Pazi kwa pointi 81-73.

Nyamoko ameliambia Mwanaspoti kwamba, hawajaridhishwa na mwenendo wa matokeo wanayoyapata kutokana na kwamba awali, kabla ya mashindano kuanza walikuwa wamepanga kutembeza vipigo dhidi ya wapinzani wao.

Alisema, baada ya kutafakari wameamua kuwaita Wakongomani Dan Kola na Vincent Marc ambao wataungana na wachezaji wengine Larry Essom na Junior Louissi ambao ni raia wa Gabon waliofika nchini kitambo kuja kuitumikia timu hiyo.

“Tunakusanya nguvu baada ya kuona mwenendo wa timu kuwa siyo mzuri katika ligi,” alisema Nyamoko na kuongeza kuwa baada ya kuwasili wachezaji hao timu hiyo itapambana kuhakikisha kwamba inazinyoosha timu zilizokuwa zinaibeza mwanzo wa msimu huu.

KIKA 04

ABC VS MCHENGA STAR

Pointi 30 zilizofungwa na Enerico Maengela wa ABC katika mchezo dhidi ya Mchenga Star ndizo zilizoifanya ABC kuibuka na ushindi wa pointi 83-60.

Kati ya pointi 30 alifunga kwa 'three point' mara 12 akiongoza pia kwa kutoa asisti mara 12, huku akifuatiwa na Antony Mvile aliyefunga 16, ilhali upande Mchenga Star alikuwa Jamal Hussein aliyefunga 15 akifuatiwa na Aloyce Boniface aliyetupia pointi 14. ABC inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania iliongoza katika robo zote nne kwa pointi 19-16, 21-18, 20-9 na 23-17.

KIKA 03

CITY, WARRIORS KAMA FAINALI

Wakati BDL ikizidi kushika kasi mchezo uliovunja rekodi ya kuwa na watazamaji wengi ulikuwa ni ule wa Stein Warriors na Dar City, ambapo tambo zilizotangulia wiki moja kabla ziliwafanya kumiminika uwanjani.

Mchezo huo uliopigwa saa 2 usiku watazamaji walianza kuingia uwanjani tangu saa 12 jioni na ilipofika saa 1 magari yalizuiwa kupaki ndani na askari aliyekuwa mlangoni ambaye alifunga geti.

Kwa upande wa watazamaji waliokuwepo uwanjani walionekana kuwa na wakati mgumu kuangalia mchezo kutokana na umati.

Katika mchezo huo Dar City iliifumua Stein Warriors kwa pointi 98-59, ambapo iliongoza katika robo zote nne kwa pointi 18-15, 22-13, 27-16 na 31- 15.

Katika mchezo huo, Jamal Marbuary wa Dar City alionekana kuisumbua Stein Warriors kutokana na jinsi alivyokuwa anapenya katikati ya walinzi na kufunga.

Marbuary ambaye ni raia wa Marekani, mbali ya kupenya mabeki pia alikuwa mwepesi kutoa asisti kwa wenzake. Nyota huyo alifunga pointi 25 kati ya hizo alifunga eneo la mtupo mmoja 'three point' mara 15 na asisti mara tisa, akifuatiwa na Amini Mkosa aliyefunga pointi 15, huku Jonas Mushi wa Stein Warriors akifunga pointi 16.

KIKA 02

ROYALS YATISHIA VIGOGO BDL

Ushindi wa Tausi Royals wa pointi 151-4 dhidi ya Kurasini Divas umewatia hofu vigogo wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (WBDL), huku hofu ikitokana na kasi ya timu hiyo inayoendelea nayo katika mashindano hayo.

Royals inayocheza msimu wa pili itacheza na vigogo ambao ni Vijana Queens, Juni 7; Jeshi Stars, Julai 27; DB Lioness, Agosti 2 na JKT Stars itakayopigwa Agosti 9.

Mchezo kati ya Royals na Kurasini Divas uliofanyika katika Uwanja wa Donbosco Upanga uliishuhudia Royals ikipambana kutumia upungufu wa Divas kutokana na kucheza mchezo laini na kufanikiwa kuibana kwenye mstari unaogawa uwanja, jambo lililoifanya iongoze katika robo ya kwanza kwa pointi 40-1. Robo ya pili Royals iliipeleka puta Divas na hadi ilipomalizika ilikuwa mbele kwa pointi 43-0.

Katika robo ya tatu iliongoza tena kwa pointi 46-2 na ile ya nne ikapata pointi 22-1. Kwenye mchezo huo Juliana Sambwe aliongoza kwa kufunga pointi 30 akifuatiwa na Rehema Joseph aliyetupia 20 huku Asnat Mohamed wa Divas akiambulia pointi tatu.