Kipigo cha Yanga, chatimua makocha Simba

Saa chache tu tangu ipokee kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa Yanga, mabosi wa klabu ya Simba leo Novemba 7 imefikia makubaliano ya kuachana na Kocha Roberto Oliveira 'Robertinho' na kocha wa viungo Corneille Hategekimana.
Taarifa kutoka klabu hiyo inasema "Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza cha Simba, Roberto Oliveira (Robertinho) na kocha wa viungo, Corneille Hategekimana”.
“Uongozi wa klabu ya Simba unawashukuru makocha hawa kwa mchango wa ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.”
Timu hiyo itakuwa chini ya kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Selemani Matola huku mchakato wa kutafuta makocha wapya ukiendelea.