Kimwaga: Jamani eehe, hii sasa inatosha!

STRAIKA wa Azam FC, Joseph Kimwaga

STRAIKA wa Azam FC, Joseph Kimwaga ametamka maneno mazito akisema, majeraha anayopigania yaponde hivi sasa, ndiyo yatakuwa yake ya mwisho kwa sababu mateso aliyoyapata, yanatosha.

Kimwaga ambaye sasa, anapata matibabu na mazoezi maalumu katika hospitali moja maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam amesema, anapata ushujaa wa kutamka hayo kwa sababu njia ya mafanikio ameshaiona.

"Kwa uwezo wa mwenyezi Mungu, imani yangu ni kwamba, maumivu haya ninayougua, hakika yatakuwa ya mwisho kwangu, jamani kama ni majeraha sasa inatosha, nianze kufanya kazi"alisema Kimwaga ambaye aliumia wakati wa maandalizi ya ligi kuu ikiwa ni mara ya pili.

Mara ya kwanza aliumia goti akafanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini na Septemba mwaka huu, alipata tena maumivu ya goti akapelekwa  Afrika Kusini na kufanyiwa upasuaji .

Amesema, alitakiwa kurudi uwanjani mwezi Desemba, lakini jopo la madaktari wake wa Azam pamoja na uongozi, wamekubaliana arudi Januari mwakani ili apone kabisa majeraha yake.