Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilichomkuta Pacome, Aucho

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amefunguka wengi hawakufahamu kilichokuwepo nyuma ya pazia kwa viungo wao wawili, Pacome Zouzoua na Khalid Aucho kwenye mchezo dhidi ya CR Belouizdad ya Aljeria, Februari 24, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ally amesema nyota hao walicheza mchezo huo huku wakiwa na majeraha waliyoyapata siku moja kabla ya mchezo huo wakiwa mazoezini na kuleta sintofahamu kwa viongozi.

Hata hivyo, amesema viongozi walitulia baada ya nyota hao kuwahakikishia wako sawa na watacheza mchezo huo na mashabiki waliona kile walichokionyesha licha ya kutokujua kama walikuwa majeruhi.
Amesema kilichofanywa na Pacome wanakiheshimu kwani hakuwa sawa ila alijitoa kwa asilimia zote kuhakikisha timu yake inashinda na alicheza kwa asilimia 50 tu za uwezo wake.
Kwa upande wa Aucho amesema aliumia kama Pacome lakini aliwahakikishia atacheza ili kuwapa furaha mashabiki wao.
Ameeleza haikuwa rahisi kwa wao kama viongozi kulipokea hilo la majeruhi hao, lakini mambo yalikuwa sawa na wachezaji hao walirejea katika hali zao za kawaida na kucheza vizuri.
"Mechi kubwa kama ile kumkosa Pacome ingekuwa habari mbaya sana, lakini alisema ni lazima atacheza na hakuna kitakachomzuia kwani ile ni siku yake, vivyo hivyo kwa Aucho," amesema Ally na kuongeza wachezaji wa Yanga wameacha deni kwa mashabiki wao la kufika uwanjani kwa wingi kila inapocheza kwani itawasaidia kufanya vizuri, akisisitiza wafanye hiyo kwenye mechi za robo fainali ambazo ni muhimu kwao kupata matokeo mazuri.
Katika mchezo huo, Pacome  ambaye mchezo huo ulipewa jina lake 'Pacome Day', alionyesha kiwango bora na kusababisha bao kwa asisti aliyoitoa kwa Kennedy Musonda, huku Aucho akiwa mhimili mkubwa kwenye safu ya kiungo ya timu hiyo ya Wananchi.