Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kile kiatu cha England kitabebwa na mastaa hawa

Muktasari:

  • Chelsea na Watford nazo zimeshinda mechi nne za mwanzo kwenye ligi hiyo kufanya mchakamchaka wa kuwania ubingwa wa msimu huu kuwa na mvuto wa kipeke yake. Wakati ikitazamwa vita ya kuwania ubingwa, kuna vita nyingine ya Kiatu cha Dhahabu inakuja.

LIGI Kuu England kumenoga. Liverpool imeshusha vipigo kwenye mechi zake zote nne ilizocheza hadi sasa na hivyo kufikisha pointi 12.

Chelsea na Watford nazo zimeshinda mechi nne za mwanzo kwenye ligi hiyo kufanya mchakamchaka wa kuwania ubingwa wa msimu huu kuwa na mvuto wa kipeke yake. Wakati ikitazamwa vita ya kuwania ubingwa, kuna vita nyingine ya Kiatu cha Dhahabu inakuja.

Mastaa wanaopewa nafasi ya kubeba tuzo hiyo wote wameshaanza kuonyesha makali yao ya kutupia wavuni, kitu kinachofanya msimu huu patachimbika. Inaelezwa hivi, kuna wachezaji sita ambao watachuana jino kwa jino kwenye kuwania tuzo ya ufungaji bora ya Ligi Kuu England baada ya msimu uliopita kunaswa na Mohamed Salah, ambaye alikomesha ubabe wa Harry Kane, ambaye alibeba kwa misimu miwili mfululizo tuzo hiyo.

Hii hapa orodha ya wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kuwania Kiatu cha Dhahabu cha Ligi Kuu England msimu huu.

Sadio Mane – Dakika 342, mabao 4

Kwenye Ligi Kuu England, staa wa Liverpool, Sadio Mane kwa sasa ndiye kinara wa mabao, akiwa ameweka kwenye kamba mara nne. Mane amefunga mabao hayo baada ya kucheza dakika 342, huku akipiga jumla ya mashuti tisa na sita tu ndiyo yaliyolenga goli. Staa mwingine aliyefunga mabao manne ni Aleksandar Mitrovic wa Fulham, ambaye amefunga idadi hiyo baada ya kucheza dakika 360, akipiga mashuti 16 na tisa tu yakilenga goli.

Sergio Aguero – Dakika 335, mabao 3

Manchester City ipo siriazi kwenye mpango wake wa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, ikiwa imekusanya pointi 10 kwenye mechi zake nne ilizocheza hadi sasa. Straika wake, Sergio Aguero ameshatupia wavuni mara tatu baada ya kucheza dakika 335 kwenye ligi hiyo msimu huu. Aguero ameasisti mara moja pia, akipiga mashuti 15 na sita tu ndiyo yaliyolenga golini.

Romelu Lukaku – Dakika 293, mabao 3

Straika Romelu Lukaku juzi Jumapili alifunga mara mbili kuisaidia Manchester United kushinda 2-0 dhidi ya Burnley na kupunguza presha ya mambo mabaya kwao msimu huu. Hadi sasa, Lukaku amefikisha mabao matatu baada ya kucheza kwa dakika 293. Kwenye Ligi Kuu England msimu huu, Lukaku amepiga mashuti 11 na manane ndiyo yaliyolenga kwenye magoli ya wapinzani.

Mohamed Salah – Dakika 338, mabao 2

Kinara wa mabao wa msimu uliopita kwenye Ligi Kuu England, Mohamed Salah bado hajaanza kuonyesha makali yake sana baada ya kufunga mabao mawili tu katika dakika 338 alizocheza hadi sasa kwenye ligi hiyo msimu huu. Salah amehusika pia kwennye asisti moja, huku akipiga mashuti 12 na saba tu ndiyo yaliyolenga magoli ya wapinzani.

Harry Kane – Dakika 358, mabao 2

Supastaa wa Tottenham Hotspur, Harry Kane msimu huu alivunja mwiko wake wa kufunga bao Old Trafford wakati alipoongoza mashambulizi kuichapa Manchester United 3-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England. Kwenye ligi ya msimu huu, Kane amefunga mabao mawili hadi sasa baada ya kucheza kwa dakika 358. Amepiga pia asisti moja, huku mabao hayo akifunga kwa mashuti yake matatu yaliyolenga goli kati ya maneno aliyopiga kwenye ligi hiyo.

Pierre-Emerick Aubameyang

Staa wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang amebeba tuzo kibao za ufungaji bora huko kwenye Bundesliga na baada ya kutua kwenye Ligi Kuu England amedaiwa atakuja kuleta upinzani mkali kwenye vita ya kuwania Kiatu cha Dhahabu. Straika huyo wa Arsenal hadi sasa ameshatupia wavuni bao moja baada ya kucheza mechi zote nne ilizocheza timu hiyo ya Emirates, lakini mashabiki wake wanaamini ni suala la muda tu, kabla ya kuanza kutupia katika kila mechi.

Wachezaji wengine

Mchakamchaka wa kuwania Kiatu cha Dhahabu cha Ligi Kuu England unadaiwa utakuwa na changamoto nyingi kutokana na kuwapo kwa wachezaji wengine wenye uwezo wa kufunga mabao na kama wakiendelea na kasi waliyoanza nayo, basi kwenye Ligi Kuu England msimu huu patachimbika.

Baadhi ya wachezaji hao ni Pedro wa Chelsea mwenye mabao matatu, huku wengine wenye idadi kama hiyo ya mabao ni Lucas Moura wa Spurs, Roberto Pereyra, Glenn Murray wa Brighton na Richarlison wa Everton.