Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikwete afunguka usajili wachezaji, kocha Yanga

Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akizungumza kwenye mkutano Mkuu wa Yanga. Picha na Michael Matemanga

Muktasari:

ALIYEKUWA Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewataka uongozi wa Yanga kuwa makini katika upande wa kutafuta makocha na wachezaji wa timu hiyo.

ALIYEKUWA Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewataka uongozi wa Yanga kuwa makini katika upande wa kutafuta makocha na wachezaji wa timu hiyo.

Kikwete ameyasema hayo wakati aliokuwa amepewa nafasi ya kuzungumza kama mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa klabu ya Yanga.

"Muwe makini kutafuta kocha na wachezaji, mabadiliko ya mara kwa mara yanaweza yakawa mazuri lakini pia yakawa mabaya," alisema Kikwete.

Kikwete amesema umakini unahitajika eneo hilo ili inabidi wawe makini na sio kubadili kocha katikati ya msimu au kuachana na wachezaji mapema.

Wanachama wa Yanga wakinyosha mikono kama kukubali mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji na mabadiliko ya katiba katika mkutano mkuu wa klabu hiyo.Picha na Michael Matemanga

Pia Kikwete aliwataka wanachama wawe na subira kwa wachezaji na makocha wanaoenda Yanga.

"Wanachama pia muwe na subira, timu haiwezi kujengwa kwa haraka, lazima wote wazoeane ili timu iwe bora," alisema Kikwete.

Kikwete pia aliwaambia Uongozi wa Yanga kuhakikisha wanawahudumia wachezaji wa Yanga kwa kuwapa stahiki zao kwa wakati.

"Wachezaji wapewe mishahara, posho zao kwa wakati hiyo itaondoa masuala ya kusema wanahujumu timu, Ng'ombe analishwa ili atoe maziwa," alisema Kikwete.

Kikwete ameongeza akisema;"Msipofanya hayo mtakuwa watu wa kamati ya ufundi na sio kamati ya benchi la ufundi, mambo hayo sio mazuri na ukiyaendekeza hautofikia mafanikio na uwekezaji mzuri kwenye timu ndio unaleta mafanikio."