JK: Wanaogeuza klabu Mkukuta sio poa

Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akizungumza kwenye mkutano Mkuu wa Yanga. Picha na Michael Matemanga
Muktasari:
Rais wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewapa makavu viongozi wanaotumia klabu kama sehemu yao ya kupata pesa.
Rais wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewapa makavu viongozi wanaotumia klabu kama sehemu yao ya kupata pesa.
Amesema sio poa baadhi ya viongozi kuzifanya klabu kuwa Mkukuta wao na pesa za klabu kwenda kwenye matumbo yao.
"Nimefurahishwa na ajenda ya bajeti ya Yanga ya mwaka huu, lazima mjue mnataka kufanya nini, gharama yake kiasi gani na mtazipata wapi,".

"Msolla na uongozi wako mnaongoza vizuri, niwapongeze na muendelee na utaratibu huu wa kutoa taaarifa ya mapato na matumizi, na taarifa ya hesabu zilizokaguliwa na watu wenye taaluma sio na makanjanja.
Amesems kama hilo haliko kwenye katiba ya Yanga waliweke na wanachama wasimamie bila woga, vinginevyo watakuwa wanaambiwa tu, kuendesha timu kazi.
"Mliyempa uongozi asigeuze klabu mali yake, anawajibu kuongoza na kuwajibika kwa waliomchagua," amesema.