Kikosi kizima cha Dodoma Jiji hiki hapa

KLABU ya Dodoma Jiji iliyopanda Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 imekamilisha usajili wa nyota wao huku ikitangaza rasmi kikosi chao chenye nyota 26 kitakachotumika ndani ya timu hiyo.
Dodoma Jiji moja ya timu zilizopanda Ligi Kuu msimu huu, kimejiimalisha vilivyo kuhakikisha kinakuwa na ushindani mkubwa katika ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Septemba 6 mwaka huu.
Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo leo kwenye mitandao ya kijamii; Makipa ni Hussein Masalanga, Emmanuel Mseja na Aron Kalambo.
Kwa upande wa mabeki ni Anderson Solomon, Abubakar Ngalema, Ibrahim Ngecha, Mbwana Kibacha, Hassan Kapona, George Wawa, Jukumu Kibanda, Augustino Ngata pamoja na Justine Omary.
Viungo watakaoitumikia timu hiyo ni Rajabu Seif, Steven Mganga, Jamal Mtegeta, Omary Kanyoro, Deus Kigawa, Salim Hoza, Cleophace Mkandala, Peter Mapunda na Dickson Ambundo.
Huku washambuliaji wanaotumainiwa kusumbua nyavu za wapinzani ni Anuary Jabir, Khamis Mcha, Santos Thomas, Sif Karie na Michael Chinedu.