Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kihimbwa hataki kumaliza kinyonge

KIHIMBWA Pict

Muktasari:

  • FG imebakiza mechi dhidi ya JKT Tanzania, Coastal Union na Azam  kabla ya kufunga msimu na Kihimbwa alisema anatamani angalau apate zaidi ya bao moja ili kumaliza msimu akiwa na mabao matano.

WINGA wa Fountain Gate, Salum Kihimbwa amesema licha ya msimu mbaya akishindwa kufikia lengo la kufunga mabao 10 na asisti 10 kama alivyokuwa amepanda awali, lakini kwa mechi tatu zilizobaki kabla ya Ligi Kuu kufikia tamati, amepania kufanya kitu ili asimalize kinyonge.

FG imebakiza mechi dhidi ya JKT Tanzania, Coastal Union na Azam  kabla ya kufunga msimu na Kihimbwa alisema anatamani angalau apate zaidi ya bao moja ili kumaliza msimu akiwa na mabao matano.

Kihimbwa hadi sasa amefunga mabao manne, asisti tano alisisitiza hataki kutoka kapa katika mechi zilizosalia ingawa maamuzi ya nani acheze yapo mikononi mwa kocha.

"Sijaweza kuyatimiza malengo yangu ila bado nina nafasi ya kufanya kitu kingine zaidi katika mechi zilizosalia, angalau nikipata zaidi ya bao moja na asisti litakuwa jambo zuri kwangu," alisema Kihimbwa anayetaja 2018 ulikuwa msimu bora kwake akiwa Mtibwa Sugar ilichukua ubingwa wa FA na alimaliza na mabao saba na asisti 10.

Mbali na hilo alisema msimu huu umekuwa na ushindani mkali, unaotafsiri baada ya miaka mitatu Tanzania itakuwa kati ya nchi za Afrika ambazo zina viwango vikubwa: "Japo Ligi ya Tanzania kwa sasa ipo nafasi nne kwa ubora ni nzuri, kwa ushindani uliopo mbeleni tunaweza kupanda juu zaidi."

Fountain kwa sasa inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 29 ikishinda mechi nane kati ya 27 ilizocheza, ikitoka sare tano na kupoteza 14 ikifunga mabao 29 na kufungwa 51 ikiwa ndiyo timu yenye ukuta mwepesi msimu huu ikiipiku hadi KenGold ilishuka daraja ilifungwa mabao 50 katika mechi 27.