Kihimbwa ajifunga mwaka Mashujaa

Muktasari:
- Kati ya wachezaji waliomalizana nayo ni winga Salum Kihimbwa aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo. Msimu uliopita alimaliza na mabao manne na asisti tano akiwa na KenGold.
TIMU mbalimbali zinaimarisha vikosi kwa kuongeza sura mpya kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, miongoni mwazo ni Mashujaa ambayo tayari imewasainisha baadhi ya wachezaji.
Kati ya wachezaji waliomalizana nayo ni winga Salum Kihimbwa aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo. Msimu uliopita alimaliza na mabao manne na asisti tano akiwa na KenGold.
Mchezaji mwingine anayetajwa kumalizana na timu hiyo ni kiungo Selemani Bwenzi aliyemaliza na mabao matano akiwa na KenGold, huku ikielezwa inafanya mazungumzo mapya na Mohamed Mussa aliyemaliza mkataba.
Chanzo cha ndani kutoka Mashujaa kilisema: “Bado tunaendelea na usajili hao ni baadhi, wengine tunaendelea kuzungumza nao. Kila kitu kikakaa sawa tutatoa taarifa.”
Alipotafutwa Kihimbwa ili kuthibitisha taarifa hizo alisema: “Ni kweli nitakuwa sehemu ya kikosi hicho msimu ujao, ila siyo mzungumzaji wa hilo kwani timu husika ndiyo inayotakiwa itoe taarifa hiyo.”
Kwa upande wa Mussa alisema: “Nimemaliza mkataba ila mazungumzo yanaendelea tukifikia makubaliano basi nitasema.”