Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kigogo wa Manji alibana wakamchinjia mbali

Athuman Kihamia(kulia) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga.

Muktasari:

  • Kwa watu wasiomfahamu, Athuman Kihamia ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, ambaye kabla ya hapo alikuwa akishika wadhifa huo kwenye halmashauri ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.

KAMATI mpya ya mashindano ya Yanga iliyoundwa na Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yussuf Manji itakuwa ya watu 18, chini ya Injinia Paul Malume akirithi mikoba ya Isaac Chanji.

Miongoni mwa majina ambayo yametajwa kuwemo kwenye kamati hiyo ni Athuman Kihamia.MwanaSpoti liliingia msituni na kumsaka mjumbe huyu ambaye ni miongoni mwa watu waliopewa dhamana nzito ya kuhakikisha Yanga inaendeleza ubabe wake kwenye medani ya soka nchini.

Kihamia ni nani?

Kwa watu wasiomfahamu, Athuman Kihamia ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, ambaye kabla ya hapo alikuwa akishika wadhifa huo kwenye halmashauri ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.

Kihamia ni miongoni mwa wanachama wa Yanga wanaoheshimika sana kutokana na michango yake ya mawazo hasa kwa vijana ndani ya nje ya Yanga.

Alikuwa miongoni mwa wagombea nafasi za ujumbe katika Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo uliofanyika mwezi Julai mwaka huu.

Alibana mkwanja wakamchinja

Kwa bahati mbaya, Kihamia hakufanikiwa kuingia katika majina saba yaliyounda Kamati ya Utendaji ya Yanga.

“Kikubwa ambacho naamini kiliniangusha ni kutotoa fedha kwa wapiga kura kama baadhi ya wagombea wenzangu walivyofanya.

Sikutaka kufanya jambo kama hilo. Kiongozi anayenunua madaraka hawezi kuwa na nia nzuri na Yanga kwa sababu mwisho wa siku ataitumia klabu kujinufaisha badala ya yeye kuipa maendeleo,” anasema Kihamia ambaye alishtuka kuteuliwa na Manji.

“Yanga iliasisiwa na Hayati Mwalimu Julius Nyerere  na Shekh Abeid Aman Karume. Ni sehemu ya nembo ya uhuru na historia ya nchi yetu hivyo kuna haja ya kuifanya iwe timu bora zaidi Afrika na hata duniani ili kuenzi uhuru wetu na wazee wetu.

Hivyo naamini Mwenyekiti wetu Ndugu Yussuf Manji hakukosea kuniteua kuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, na Wanayanga wataendelea kufurahi tu,” anatamba Kihamia.

Licha ya kutingwa na majukumu ya kiserikali kila mara, Kihamia ni miongoni mwa wadau wakubwa wa soka nchini. Awali aliwahi kuwa Meneja na mmoja wa walezi wa timu ya Kurugenzi ya Halmashauri ya Mufindi ya Iringa inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ngazi ya taifa.

“Baada ya kuhamishiwa kwenye Wilaya ya Kaliua kule Tabora, niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa timu ya  Rhino ya Tabora inayomilikiwa na Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) ambayo nayo ipo kwenye Ligi Daraja la Kwanza Taifa,” anasema Kihamia.

Pia kwa juhudi zake binafsi alianzisha na kuisimamia timu ya  Wananchi  ya Kaliua city aliyoitoa madaraja ya chini hadi ikafanikiwa kucheza fainali za soka ngazi ya mkoa wa Tabora.

Mkakati wake

“Kikubwa ambacho nimepanga kukifanya ni kushirikiana vyema na uongozi chini wa Manji, wajumbe wenzangu pamoja na wanachama kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi sio kwenye ligi ya ndani pekee bali na mashindano ya kimataifa.

“Pia ninataka kuwa daraja la kuwaunganisha mashabiki, wapenzi na wanachama wa Yanga wa kanda ya Kaskazini kwa mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro na wenzao Tanzania nzima,” anasema Kihamia.

“Nia yetu ni kuiona Yanga inafanya vizuri kila siku. Hilo haliwezi kutimia kama tumetengana. Uongozi unafanya kazi nzuri ambayo tunatakiwa tuiunge mkono kwa kushirikiana. Kila Mwanayanga atimize wajibu wake kwa timu, tutasonga mbele,” anamalizia Kihamia.