Kibu kuongoza mashambulizi Simba dhidi ya Wamalawi

Muktasari:

KOCHA mkuu wa Simba, Juma Mgunda ameamuanzisha mshambuliaji wake, Kibu Denis katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets kutoka Malawi.

KOCHA mkuu wa Simba, Juma Mgunda ameamuanzisha mshambuliaji wake, Kibu Denis katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets kutoka Malawi.

Mchezo huu unaopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ni wa marudiano baada ya mechi ya kwanza iliyopigwa Septemba 11, Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ikiwa ugenini.

Katika eneo hilo Kibu atapata msaada wa karibu na viungo washambuliaji, Clatous Chama na Moses Phiri ambaye mchezo wa kwanza alikuwa mwiba kwa Wamalawi hao.

Kikosi kamili kinachoanza ni, Aishi Manula, Israel Mwenda, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Kennedy Juma, Henock Inonga, Sadio Kanoute, Kibu Denis, Mzamiru Yassin, Moses Phiri, Clatous Chama na Augustine Okrah.

Wachezaji wa akiba ni, Beno Kakolanya, Erasto Nyoni, Mohamed Ouattara, Jonas Mkude, Pape Sakho, Nelson Okwa, Dejan Georgijevic, John Bocco na Peter Banda.

Simba inaingia katika mchezo huu ikihitaji sare au ushindi wa aina yoyote ili kufuzu hatua inayofuata.