Kelvin John: Haikuwa kazi nyepesi

JINA la kinda fundi wa mpira, Kelvin Pius John (18), lilianza kujulikana kwa Watanzania kupitia madini ya mguu wake, wakati anatumika kwenye timu za vijana U- 17 na U-20.

Kipaji chake kimempa dili katika timu ya Genk ya Ubelgiji alikosaini mkataba wa miaka mitatu ikiwa ni baada ya kuanzia kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji cha Football House kilichopo Bwiru Jijini Mwanza ambacho alikuwa akikitumikia kabla ya kujiunga na Kituo cha Brooke House College Football Academy kilichopo Mji wa Leicester nchini Uingereza.

Mwanaspoti limefanya mahojiano maalumu na Kelvin anayefahamika na wengi kama, Mbappe ikiwa ni siku chache tangu asaini mkataba na Genk, klabu aliyoichezea nyota wa kimataifa na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta. Endelea naye...!


GENK ZAIDI YA NDOTO

“Namshukuru Mungu hili limemnalizika salama na mimi rasmi ni mchezaji halali wa KRC Genk ya nchini Ubelgiji ni zaidi ya ndoto kwangu kutua hapa na kudumu miaka mitatu nawaomba watanzania kuniunga mkono kwa kunipa ushirikiano ili niweze kufikia malengo,” anasema.

“Ni taarifa ambayo haikuwa Suprised kwangu kujiunga na Genk nilikuwa naifahamu mwaka mmoja nyuma nilishindwa kujiunga kutokana na umri lakini baada ya kuambiwa wakati ni sasa nilifurahi sana kwani sikutegemea kama nafasi yangu mwaka mmzima ilibaki,” anasema.


KIOO CHANGU NI

SAMATTA

Mbwana Samatta ndo ‘role model’ wangu, hadi sasa hivi naiga vitu vingi kutoka kwake akiwa uwanjani jinsi anavyoisaidia timu yake na anavyoisaidia timu ya taifa.

“Genk ni timu yangu mpya na ni timu ambayo amepita kaka yangu Sammata aimemfungulia milango ya mafanikio natamani kufika mbali zaidi ya alipo yeye ndio maana nimekuwa nikimfuatilia pia amekuwa akinishauri na kunitaka nipambane zaidi nazani hicho ndio kitanivusha mbali zaidi yake,” anasema.


SAMMATA

AMTOA CHOZi

“Tunaamini uwezo wako weka juhudi katika kazi zako naamini utafanya vizuri,” anasema ni maneno machache ambayo hayakumchosha zaidi yalimtoa machozi baada ya kuyasoma kwenye ujumbe mdogo wa meseji kutoka kwa kaka yake Samatta baada ya kutangazwa rasmi kujiunga na Genk.

Anasema mbali na ujumbe huo kaka yake amekuwa kiongozi mkubwa kwa kumuunganisha na viongozi sambamba na wachezaji wakubwa wa timu hiyo ili waweze kumuongoza vyema.

“Nimepokelewa vizuri Genk nimepewa ushirikiano wa kutosha sijaitwa Kelvin nimekuwa nikitwa mdogo wa Sammata wananiamini wanajua nitafanya makubwa zaidi ya kaka Yangu namuomba Mubngu asimame upande wangu nitimize hili wanalolitegemea,” anasema.


BARIDI CHANGAMOTO

“Nimekaa nchi mbili tofauti na zote changamoto yake ni hari ya hewa kwasababu hata sasa nipo Genk huku kuna baridi sana kitu ambacho kinaniathiri japo naamini katika mabadiliko ipo siku nitakaa sawa na kuona ni jambo la kawaida tu kwenye maisha yangu ya kawaida,” anasema.

“Nimekulia Mwanza na mara nyingi nimekuwa nikifikia huko muda mwingi wa mapumziko hari ya Mwanza huwezi kufananisha na huku ni tofauti kabisa huku baridi muda wote asubuhi, mchana na jioni naamini ntazoea kwani sina ninachokipoteza nataka kufikia malengo,” anasema.


MIAKA MITATU BAADAE

“Hakuna mtu aliyekuwa anategemea kusikia au kuniona nikicheza Genk kwa umri huu nilionao juhudi, Heshima na mapenzi ya kazi ninayoifanya ndio siri ya mafanikio japo si mwisho wangu huu najiona mbali zaidi baada ya miaka hii mitatu niliyosajiliwa hapa,” anasema.

“Katika mpira huwezi kusema mimi ntakuwa wapi au najiona wapi lakini kwa upande wangu juhudi zangu zitanifanya niwe sehemu bora na ya ushindani zaidi baada ya miaka mitatu,” anasema kinda huyo.


MALENGO YAKE

“Mimi maisha yangu ni mpira hivyo nategemea kupata mafanikio kupitia soka. Kikubwa ninachomuomba Mungu ni kuniepusha na matatizo yanayotokana na mpira, aidha kwa kuvunjika au kusimamishwa kujihusisha na soka kwasababu malengo yangu ni kupambana kucheza soka vizuri ili niweze kucheza Ulaya,” anasema Kelvin na kuongeza;

“Genk ni njia ya kusogea mbali zaidi umri wangu bado unaniruhusu kucheza kikubwa ni kuepukana na changamoto zitakazoniweka nje ya soka natamani kufika mbali zaidi ya hapa japo pia ilikuwa ni ndoto yangu kuwaza kucheza sasa imetimia naamini milango mingine itafunguka zaidi.”

“Hakuna mchezaji mwenye malengo ya kuendelea kubaki Tanzania. Kila mmoja anatamani kufika mbali zaidi kwa kucheza soka la kulipwa, hivyo kutokana na changamoto hiyo ili niweze kuifikia ndoto yangu ninahakikisha napambana na kutokukubali kukatishwa tamaa na kuamini nina uwezo na ninaweza kufika ninapopataka,” anasema.


SIKU MOJA KABLA YA MECHI

Anasema kitu cha kwanza anamuomba Mungu amuepushe na changamoto ya kuumia akiwa mchezoni na pia anamuomba amfanikishie aweze kufunga yeye kama mshambuliaji kwani ndio kazi yake hawezi kujisikia vizuri akikosa nafasi ya kufunga au kutengeneza nafasi ya timu yake kupata bao.

“Mshambuliaji ni mchezaji muhimu uwanjani japo kila mchezaji akipata nafasi anaweza akafunga kwa upande wangu ili nimalize dakika zote 90 kwa amani basi nilazima nitengeneze nafasi au nifungi nisipofanya ivyo nakosa amani naona kama sijatendea haki umuhimu niliopewa uwanjani,” anasema.


JEZI NAMBA 10

Wachezaji huchagua namba za jezi zao mgongoni kutokana na sababu mbalimbali na kwa Kelvin hali ni hiyo hiyo.

“Navaa jezi namba 10 kwasababu ndio tarehe yangu ya kuzaliwa. Huwa naitumia kama kumbukumbu. Niliamua kuchagua tarehe na sio mwezi kwa sababu kwa upande wa mama yangu lilikuwa ni tukio zuri kunipata mimi katika tarehe hiyo,” anasema.