Kaze amrudisha Carlinhos Yanga ikiwakaribisha Namungo

Kaze amrudisha Carlinhos Yanga ikiwakaribisha Namungo

Muktasari:

  • Yanga inashuka Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wake wa 10 wa ligi ikiwakaribisha Namungo FC ya Lindi huku badiliko kubwa likiwa kurejea katika kikosi cha kwanza kwa kiungo Carlos Carmo 'Carlinhos' ambaye alikosekana kwa mechi tano zilizopitaa akiwa majeruhi.

Kocha Mkuu wa Yanga amemrudisha katika kikosi cha kwanza kiungo  Carlos Carmo 'Carlinhos' wakati timu yake ikiwakaribisha Namungo ya Lindi mchezo utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa chache zijazo.

Hata hivyo Kaze ambaye kikosi chake hakijapoteza mchezo wowote mpaka sasa hajafanya mabadiliko yoyote katika safu yake ya ulinzi akiendelea kuwaamini kipa Metacha Mnata,beki wa kulia akiwa Kibwana Shomari,kushoto Yassin Mustapha wakati mabeki wa kati wakiwa nahodha mkuu Lamine Moro na msaidizi wake Bakari Mwamnyeto.

Mbali na ukuta huo kuwa haujapoteza mchezo wowote mpaka sasa lakini rekodi nyingine bora ni kuwa wameruhusu mabao machache zaidi wakiruhusu mabao matatu pekee katika mechi zao 9 zilizopita.

Safu ya kiungo kiungo Mkongomani Mukoko Tonombe na Feisal Salum wameendelea kuaminiwa na Kaze wakisaidiwa na Tuisila Kisinda na Farid Mussa ambao watakuwa wakitokea pembeni.

Safu ya ushambuliaji Michael Sarpong ndio ataongoza kazi ya kutafuta mabao sambamba na Carlinhos ambaye mechi yake ya mwisho kabla ya kurejea leo alifunga na kutengeneza bao moja wakati Yanga ikiwachapa Coastal Union kwa mabao 3-0 katika Uwanja huohuo.

Kwenye benchi Kaze amewapa nafasi kipa Ramadhan Kabwili,maqbeki Adeyun Saleh,Said Makapu,viungo Zawadi Mauya,Deuse Kaseke na washamabuliaji Ditram Nchimbi na Yacouba Sogne.

Endapo Yanga itashinda mchezo huo dhidi ya Namungo utawafanya kupanda kileleni na kuongoza msimamo wa ligi wakifika pointi 27 wakiwashusha Azam FC ambao jana walikubali kichapo cha bao 1-0 ugenini dhidi ya KMC.

...........................................

Na Khatimu Naheka