Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaze aleta fundi mwingine Yanga

KOCHA wa Yanga, Mrundi Cedrick Kaze jana aliwafanyia usaili makocha wanne wazawa, ili kupata mrithi wa Juma Mwambusi aliyeng’oka Jangwani.

Mwambusi inaelezwa kwamba ameomba kukaa pembeni kutokana na matatizo binafsi ambayo hata hivyo hayajafafanuliwa ingawa yeye alipotafutwa jana hakupenda kufafanua.

Mwanaspoti limejiridhisha kwamba Yanga imewafanyia usaili makocha wanne wazawa jana ambao kati ya sifa zao ambazo Kaze alizitaka wawe wanajua Kiingereza, uelewa wa wachezaji wazawa, leseni nzuri pamoja na mapenzi na klabu.

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti lilizipata ni kwamba makocha hao ni Shabaan Ramadhani, Maalim Saleh ‘Romario’, Nizar Khalfan na Mohammed Adolf Rishad. Uamuzi wa nani atachukua kiti cha Mwambusi utatolewa muda wowote na Yanga baada ya kupata ruksa ya Kaze.

Kocha huyo anatazamiwa kuanza kazi Jumatatu timu hiyo itakapoanza mazoezi Jijini Dar es Salaam.

Yanga wanaingia kambini Jumapili ambapo pia staa wao mpya, Fiston Abdulrazak anatazamiwa kutua siku hiyo tayari kujiandaa na Ligi Kuu mzunguko wa pili.

Mbali na Fiston kwenye dirisha dogo pia Yanga imemsajili, Said Ntibazonkiza na Dickson Job.

Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara iliyosimama kwa muda, ikiwa na pointi 44, Simba 35 na Azam 32. Yanga haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa licha ya kucheza mechi 18.