Kaze afanya badiliko moja tu kuivaa Azam

Kikosi cha Azam FC kilikuwa cha kwanza kuingia Uwanja wa Amaan kukabiliana na Yanga katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi huku Yanga ikiwa na badiliko moja la mchezaji kwenye kikosi chao cha leo.

Mechi hiyo inatarajia kuanza saa 10:15 jioni ambapo Azam waliingia saa 14:30 mchana wakati Yanga wakiingia saa 9:00 alasiri kwenye Uwanja wa Amaan kisiwani Unguja, Zanzibar.

Azam FC waliposhuka kwenye gari yao wachezaji ambao hawapo kikosini kama kipa David Kisu walikwenda kukaa jukwaani moja kwa moja.

Hata hivyo, kocha wa Yanga amefanya badiliko moja tu kwenye kikosi cha kwanza ambapo amemuanzisha Michael Sarpong akimuacha Paul Godfrey.

Kikosi cha leo Jumatatu kinaongozwa na Faruk Shikhalo, Kibwana Shomary, Adeyun Saleh, Said Juma, Abdallah Shaibu, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda, Zawadi Mauya, Sarpong na Haruna Niyonzima.

Mechi hiyo itaamua mshindi atakayetinga hatua ya Fainali ya mashindano hayo ambayo yanafikia kilele keshokutwa Jumatano, Januari 13.

Kikosi cha Azam FC kilicho chini ya kocha George Lwandamina kinaongozwa na Wilbol Changarawe, Nico Wadada, Bruce Kangwe, Daniel Amoah, Abdallah Kheri, Frank Domayo, Obrey Chirwa, Salum Abubakary, Mpiana Monzinzi, Never Tigere na Iddi Nado.