Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kauli ya TPLB ligi ikielekea ukingoni

TPLB Pict

Muktasari:

  • Kaimu Ofisa Habari wa TPLB, Yahya Abushehe amesema kila msimu ubora wa mechi za Ligi Kuu unaongezeka, jambo linalothibitisha Tanzania ni kati ya nchi zenye ligi nzuri na bora Afrika.

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imezungumzia ushindani mkali katika Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2025-2026 unaokwenda kuhitimishwa Juni 30, 2026 ikisema unatoa taswira ya ujao wa 2026-2027 kuzidi ubora na ugumu.

Kaimu Ofisa Habari wa TPLB, Yahya Abushehe amesema kila msimu ubora wa mechi za Ligi Kuu unaongezeka, jambo linalothibitisha Tanzania ni kati ya nchi zenye ligi nzuri na bora Afrika.

“Ligi ilikuwa nzuri na yenye ushindani wa hali ya juu, umezidi kuliko ambavyo ulikuwa msimu uliopita, hilo linatoa taswira ya jinsi ambavyo ujao wa 2026-2027 timu zitakuwa zimejipanga na zitakuja na chalenji ya ushindani wa juu zaidi,” amesema Abushehe na kuongeza;

DARA 02

“Kama TPLB tunafurahia kuona maendeleo ya mpira wa miguu nchini yanazidi kukua na tunafanya tathmini ya kipi kiboreshwe zaidi ili kuendelea na ubora huu wa ligi.”

Katika hatua nyingine, kiongozi huyo amesema kuelekea mechi za mwisho kuhitimisha msimu zitakazochezwa Juni 30, mwaka huu zote kuanzia saa 10:00 jioni, wanafahamu ushindani uliopo kuanzia kwa timu zinazowania ubingwa, kutoshuka daraja na wachezaji upande wa tuzo binafsi za ufungaji bora na asisti.

Katika hilo, Abushehe amesema: “Kwa sababu bingwa atapatikana mechi za mwisho, hivyo timu itakayofanikiwa kuchukua ndio tutakayoipelekea kombe, tumejiandaa kwa kila kitu tunasubiri siku ifike ili tuweze kuhitimisha msimu salama.”

MABU 01

Yanga inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 72 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 70, timu hizo zinapambania ubingwa ambapo Yanga inaonekana kuwa karibu zaidi kwani ushindi au sare unawafanya kufikia malengo hayo kutokana na uwiano mzuri wa mabao ilionao.

Ili Simba iwe bingwa kwa mara ya kwanza baada ya misimu minne kupita, inapaswa kuifunga KMC, kisha Yanga ipoteze mbele ya JKT Tanzania.

Katika upande mwingine, Mtibwa Sugar inaifuata Namungo huku zote zikihitaji ushindi kujiweka salama na hatari ya kushuka daraja.

Namungo inahitaji sare tu ili kubaki salama isiwepo hata katika mechi za mtoano kwani hivi sasa ina pointi 31, ikifikisha 32, hata Mbeya City na Prisons zikishinda mechi zao za mwisho, zitaishia 32 lakini zinahukumiwa na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Mbeya City yenye pointi 29 katika nafasi ya 13, inaikaribisha TRA United, wakati Prisons ambayo nayo ina pointi 29 ikikamata nafasi ya 14, inaifuata Mashujaa. Huku Fountain Gate yenye pointi 30 katika nafasi ya 12, inatakiwa kushinda itakapoikaribisha Singida Black Stars ili kuwa salama.