Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa wawapa saluti, Okello, Barker kunyakua tuzo za NBC PL

Muktasari:

  • Okello amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Mei wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2025/26, vivyo hivyo kwa kocha  Barker.

BAADA ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Allan Okello na kocha wa Simba, Steve Barker kupata tuzo ubora za mwezi, kulingana na kazi walizofanya, wadau wa soka wamesema wamestahili kwa jinsi walivyozisaidia timu hizo kufanya vizuri mwezi Mei.

Okello amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Mei wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2025/26, vivyo hivyo kwa kocha  Barker.

Nyota huyo raia wa Uganda alikuwa na muendelezo wa kiwango kizuri katika mwezi huo ikiwa ni pamoja na kufunga mabao tisa, asisti saba, akiwashinda katika kinyang'anyiro hicho viungo Clatous Chama wa Simba na Feisal Salum 'Fei Toto' wa Azam FC alioingia nao fainali katika mchakato wa tuzo za mwezi uliofanywa na kamati ya tuzo za Shirikisho la soka Tanzania (TFF).

Kwa mujibu wa taarifa za Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) zilisema Barker aliyeingia fainali na Florent Ibenge wa Azam na Fred Minziro wa Fountain Gate, aliiongoza timu ya Wanamsimbazi kushinda mechi tano iliyocheza na kutoka sare mmoja na kuendelea kubaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Jambo ambalo beki wa zamani wa Yanga, Oscar Joshua alisema:"Kutokana na kazi walizozifanya kwa mwezi huo Okello na kocha wa Simba, Barker wanastahili pia zinaibua ushindani wa hali ya juu."

Mwingine aliyechangia hilo ni winga wa zamani wa Simba, Emmanuel Gabriel aliyesema:"Kocha wa Simba ameibadilisha timu imekuwa katika ushindani unaochelenji ubingwa na mwezi huo timu imefanya vizuri, vivyo hivyo kwa Okello wa Yanga."

Mbali na Okello na kocha wa Simba, meneja wa Uwanja wa Airtel Singida, Omar Malule amechaguliwa kuwa meneja bora wa uwanja kwa mwezi Mei kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya mechi pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

Katika hatua nyingine Salum Mlemwa wa Gunners amechaguliwa mchezaji bora wa mwezi Mei wa Ligi ya NBC Championship 2025/26, huku Henry Mkanwa pia wa Gunners akichaguliwa kocha bora wa mwezi huo.

Mlemwa aliyeingia fainali na Richardson Ng'ondya wa Geita Gold na Maulid Shaaban wa Geita Gold, alionyesha kiwango chenye mwendelezo ikiwa ni pamoja na kufunga mabao manne kwa dakika 357.

Kwa upande wa Mkanwa aliyeingia fainali na Twaha Beimbaya wa B19 na Mbwana Makata wa Polisi Tanzania, aliiongoza timu timu hiyo kushinda mechi nne iliyocheza na kupanda kutoka nafasi ya 11 hadi ya saba katika msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC.