Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kapombe ndani Team Samatta wale Team Kiba wajipange

Muktasari:

Team Kiba na Team Samatta ni msimu wao wa pili sasa kucheza mchezo huo wa hisani kwaajili ya kuchangisha fedha zakusaidia watoto wasiojiweza kupitia taasisi yao ya SamaKiba Foundation.

Dar es Salaam. Mshambuliaji na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amemrudisha uwanjani beki wa Simba, Shomari Kapombe katika kikosi chake cha Team Samatta kinachojianda na mchezo dhidi ya Team Kiba itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Juni 2 mwaka huu.

Kapombe anatarajia kuonekana katika mchezo unaotarajia kukutanisha timu ya mashabiki wa Alikiba 'Team Kiba' na Mbwana Samatta 'Team Samatta' kwaajili ya kupata fedha za kuwasaidia watoto wasiojiweza kupitia mfuko wao wa Samakiba Foundation.

Samatta ametangaza kikosi chake akiwemo Kapombe aliyekuwa majeruhi kwa muda miezi sita sasa anatarajia kurudi tena uwanjani.

Nyota wengine walioitwa katika kikosi hicho ni pamoja na chipukizi wa Serengeti Boys, Kelvin John ambaye atasimama mbele pamoja na Samatta.

Kikosi hicho kimejaa wakongwe wengi huku Kelvin ndio mchezaji mdogo kuliko wachezaji wengine wote.

Team Samatta: Kiungo Athuman Idd 'Chuji', Shaban Chilunda, Farid Mussa, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba, Himid Mao, Mohammed Samatta, Kelvin Yondani, Thomas Ulimwengu, Erasto Nyoni na Juma Kaseja.

Wachezaji watakaocheza kikosi cha mashabiki wa Kiba 'Team Kiba' ni Aishi Manura, Abdi Banda, Agrey Morris, Abdul Kiba, Saimon Msuva, Haruna Niyonzima, Ibrahim Ajib, Said Ndemla, Mohammed Binslum, Shiza Kichuya, Emmanuel Okwi na Tundaman.