Kamwaga: msinifananishe na Manara

Thursday July 29 2021
kamwaga pic
By Mwandishi Wetu

SIKU moja baada ya kuteuliwa na uongozi wa Simba kuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Ezekiel Kamwaga amesema kuwa asifananishwe na msemaji aliyeondoka klabuni Haji Manara katika utendaji wa majukumu katika timu hiyo.

Kamwaga alisema kuwa anatambua mchango mkubwa uliofanywa na Haji Manara katika timu hiyo hivyo hapaswi kulinganishwa nae kwa kuwa kila mmoja anasifa tofauti na mwenzake

"Manara amekuwa ni mtu muhimu katika timu yetu hivyo tunapaswa kumuheshimu kwa mchango wake mkubwa alioutoa na kuacha maisha mengine yaendelee" alisema.

manara pic

Aidha Kamwaga alisema kuwa anaupongeza uongozi wa timu kwa kumpa nafasi hiyo na kuahidi kwenda na kasi ya mabadiliko ya timu hiyo kwenye uendeshaji.

"Nawashukuru bodi ya wakurugenzi kwa kuniamini kunipa tena nafasi hii, nawaahidi mashabiki wa Simba kufanya kazi kwa bidii na kuendana na mabadiliko ya kiutendaji y klabu yetu" alisema.

Advertisement

Kamwaga anachukua nafasi hiyo kwa miezi miwili baada ya Haji Manara kuamua kuacha majukumu ya kuendelea kuwa msemaji wa klabu hiyo.

IMEANDIKWA NA DAUDI ELIBAHATI

Advertisement