Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KAMARI : Souness adai kumsajili Balotelli ni bahati nasibu

Muktasari:

Mtukutu huyo ametua Anfield kwa dau la Pauni 16 milioni akitokea AC Milan kwa ajili ya kusaidia kuziba pengo la Luis Suarez aliyetimkia Barcelona baada ya kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia.

KUMSAJILI Balotelli ni bahati nasibu. Ni kama kucheza kamari. Yule jamaa hatabiriki. Kazi anayo Brendan Rodgers. Hayo ni maneno ya kocha wa zamani wa Liverpool, Graeme Souness akimuonya kocha wa Liverpool baada ya kumsajili Mario Balotelli.

Mtukutu huyo ametua Anfield kwa dau la Pauni 16 milioni akitokea AC Milan kwa ajili ya kusaidia kuziba pengo la Luis Suarez aliyetimkia Barcelona baada ya kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia.

Wakati mashabiki wengi wa Liverpool wakiamini kwamba huenda Rodgers amezichanga karata zake vizuri kwa kumchukua nyota huyo, Souness anahisi kwamba Rodgers amecheza kamari.

“Ni bahati nasibu kubwa iliyochezwa na Rodgers. Sidhani kama alilazimika kucheza bahati nasibu hii kwa sababu tayari ana kundi kubwa na zuri la wachezaji,” alisema Souness ambaye aliipa Liverpool taji la FA mwaka 1992 na amewahi kuzifundisha timu za Newcastle, Blackburn, Rangers na Southampton.

“Amani inaonekana kuwa juu kwa sasa katika timu lakini kama ilivyo kwa makocha wengi waliowahi kumfundisha Mtaliano huyo na yeye atakuwa anatumia muda mwingi kumwongelea Balotelli, atakuwa anatumia muda mwingi kumtetea yeye kuliko wachezaji wengine,” alisema Souness.

Souness aliongeza kwamba kama angekuwa kocha wa Liverpool kipindi hiki asingemchekua nyota huyo wa zamani wa Inter Milan na Manchester City. Hata hivyo mwandishi maarufu wa Gazeti la Daily Mail la Uingereza, Martin Samuel amepingana na mawazo hayo ya Souness.

“Balotelli alikuwa mkali sana katika pambano dhidi ya England Manaus. Anaweza asiwe katika daraja la Luis Suarez lakini bado ana uwezo mkubwa wa kushinda mechi peke yake. Kila timu inayohitaji ubingwa inahitaji mshambuliaji kama yeye,” alisema Samuel katika makala yake.

“Wakati mchezo wa soka ukiendelea kuzingirwa zaidi na fomesheni ya viungo watano, mechi kubwa zitaamuliwa na uwezo binafsi wa mchezaji. Hakuna shaka Balotelli anaweza kufanya jambo hilo,” aliongeza Samuel.

“Ndiyo ni bahati nasibu hata kama akimhakikishia mwajiri wake kuhusu tabia zake. Siyo kwamba anachofanya Balotelli ni tatizo, hapana, ni jinsi anavyotengeneza presha kwa kuwepo kwake.”