Kaluwa: Nitatoa ushirikiano kwa kila mmoja wetu

ALIYEKUWA mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Klabu ya Simba, Moses Kaluwa amesema ataendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wenzake licha ya kushindwa na mpinzani wake, Murtaza Mangungu.
Kaluwa amezungumza hayo ikiwa ni muda mchache tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi na Mwenyekiti wa Kamati hiyo iliyokuwa inasimamia shughuli hiyo, Boniface Lihamwike.
"Nichukue nafasi hii kuwashukuru kwa wale wote walionipa kura zao, Simba ni kubwa kuliko mtu yeyote hivyo niseme wazi kwamba nitashirikiana na viongozi wote waliokuwa madarakani."
Katika uchaguzi huo ambao matokeo yake yametangazwa Afajiri ya Januari 30, Kaluwa amepata kura 1,045 huku Mangungu ambaye alikuwa anatetea kiti chake akipata jumla ya kura 1,311.