Kahata aaga Simba

Saturday June 05 2021
kahata 1
By Thobias Sebastian

SIMBA imefikia makubaliano ya pande zote mbili kuachana na mshambuliaji wake, Mkenya Francis Kahata ambaye mkataba wake wa miaka miwili ilikuwa ukimalizika Juali 30, 2021.

Baada ya kukubaliana na Kahata, mwanzoni mwa wiki hii Uongozi wa Simba ulikubali kumlipa kila kitu ambacho alikuwa anastahili kupata katika kipindi cha mkataba wake ili kwenda kutafuta changamoto mpya.

kahata2

Kahata aliliambia Mwanaspoti, alikutana na Ofisa mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez ambaye alimueleza wamefikia maamuzi ya kuachana nae na wapo tayari kumlipa kila kitu.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram Kahata aliandika ujumbe wa kuwaaga wote aliohusika kufanya nao kazi katika kikosi cha Simba kwa muda wa miaka miwili.

Aliandika "Imekuwa ni safari ambayo ni tamu, isiyokumbukwa na yenye uchungu tangu nilipotua kwa mara ya kwanza nchi hii nzuri ya Tanzania.

Advertisement

"Nilipokea msaada mkubwa na upendo kutoka kwa timu ya watendaji wakiongozwa na Mo Dewji, wafanyikazi wa benchi la ufundi, wechezaji wenzangu na mashabiki wa Wanasimba," aliongezea

kahata 3

"Shukrani zangu zinamwendea kocha mkuu, Didier Gomes kwa kunipa nafasi ya kuwakilisha rangi nyekundu, wachezaji wenzangu kwa msaada mzuri na kila mtu aliyepanda kuwa nami katika safari yangu ndefu.

"Ninaondoka nikiwa nimeinua kichwa juu na kujivunia mafanikio yangu kwenye klabu hii. Imefikia wakati wa kuaga na kusema kwaherini nyote.

"Mwanaume anapaswa kutafuta changamoto mpya na fursa kubwa mahali pengine. Nitashukuru timu kwa kila kitu na naitakia kila la heri timu katika michezo na misimu ijayo."

"Miaka miwili ilikuwa safari. Asanteni sana Wanasimba na kila la kheri hadi siku nyingine panapo majaliwa."

kahata 4

Kahata kabla ya kuachwa katika kikosi cha Simba kabla ya miezi sita mkataba wake kumalizika aliondolewa katoka orodha ya wachezaji wa mashindano ya ndani na alibaki katika usajili wa Ligi ya mabingwa Afrika tu.

Katika mashindano ya ndani nafasi yake ilichukuliwa na Mzimbabwe Parfect Chikwende ambaye alisajiliwa kutokea FC Platinum ya nchini humo.

Advertisement