Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kagere, Morrison penalti zimewaumbua na kuwabeba Ligi Kuu Tanzania

Muktasari:

Katika mchezo huo kinara wa mabao wa Ligi Kuu, Meddie Kagere mwenye mabao 14 na Ajib Ibrahim penalti zao ziliota mbawa. Lakini kama hujui kuna wengine huko Ligi Kuu nao walichomesha.

KUNA msemo kwamba timu zinapofika hatua ya matuta, hapo shujaa anayesubiriwa ni mlinda mlango kufanya maajabu yake.
Juma Kaseja ni mmoja wa makipa ambao walipata sifa katika kuokoa michomo hiyo anapokuwa na timu ya taifa au klabu alizopita.

Mapema wiki hii, Simba ambao ni vinara wa Ligi Kuu na mabingwa mara mbili mfululizo nusura watolewe na timu ya daraja la chini kwenye kipute cha Kombe la Ligi (FA) walipotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Stand United na mchezo kuamuliwa kwa penalti.
Katika mchezo huo kinara wa mabao wa Ligi Kuu, Meddie Kagere mwenye mabao 14 na Ajib Ibrahim penalti zao ziliota mbawa. Lakini kama hujui kuna wengine huko Ligi Kuu nao walichomesha.

MEDDIE KAGERE - SIMBA
Siyo tu kinara wa kufumania nyavu. Wiki iliyopita Kagere angeongeza idadi ya mabao baada ya kupata nafasi ya kufunga kutokana na penalti aliyopiga kuota mbawa.
Penalti hiyo ilitokana na Kagere kufanyiwa madhambi na beki wa Biashara United, Derick Mussa baada ya majalo safi ya Luis Miquissone lakini kipa wa Biashara, Daniel Mgole akaidaka.
Kagere ndani ya mwaka huu amekosa penalti tatu. Alianza kukosa katika mchezo wa nusu fainali Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam kisha kwenye Ligi Kuu mbele ya Azam na mapema wiki hii mbele ya Stand United.

SIXTUS SABILO -POLISI TANZANIA
Ilikuwa Februri 11, mwaka huu, Uwanja wa Uhuru wakati Azam ikiikaribisha Polisi Tanzania na dakika ya nane, Sixtus Sabilo alipiga krosi ambayo Daniel Amoah aliunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Mwamuzi wa mchezo huo akaonyesha tuta lililopigwa na Sabilo, lakini kipa wa Azam FC, Razak Balora akapangua.

BERNAD MORRISSON - YANGA
Kipute kilipigwa Februari 15, Uwanja wa Taifa na katika dakika ya 70 Yanga ilipata penalti iliyotokana na kipa wa Tanzania Prisons, Jeremiah Kisubi kumfanyia madhambi Morrison na mwamuzi kuamuru tuta.
Morrisson alipiga
mkwaju ambao ulipaa na kufanya Yanga kuambulia alama moja katika mchezo huo uliomalizika kwa suluhu.

WAZIR JUNIOR -MBAO FC
Chipukizi huyo mwenye mabao saba hadi sasa kwenye Ligi Kuu anaingia kwenye orodha ya wachezaji waliokosa penalti msimu huu.
Wazir Jr alikosa tuta katika kipute dhidi ya Azam FC pale CCM Kirumba, Oktoba 23, mwaka jana baada ya Bruce Kangwa kuunawa mpira lakini tuta lake likapaa.

LUCAS KIKOTI -NAMUNGO FC
Kikoti ni moja ya viungo bora wazawa ambaye ameibukia Namungo FC tangu msimu uliopita akiiwezesha timu hiyo kupanda Ligi Kuu.
Lakini Februari 5, mwaka huu, Namungo FC ilibanwa mbavu wakatoka bao 1-1 na Alliance FC katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi ila mkwaju wake uliishia mikononi mwa John Mwanda.

ABASIRIM CHIDIEBELE -MBEYA CITY
Licha ya chama lake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli FC katika mchezo uliopigwa Sokoine, Mbeya, Februari 18, lakini Mnigeria huyo tuta lake liliota mbawa na kuishia kwa Deogratius Munis ‘Dida’.

HAWA WANATISHA
Baada ya kutazama wachezaji wachache ambao wamekosa penalti kwenye Ligi Kuu hadi sasa, kuna baadhi ya nyota wamekuwa moto wa kuotea mbali wanapopewa jukumu la kufunga kwa penati. Ona hawa.

PETER MAPUNDA -MBEYA CITY
Huyu jamaa noma sana anapopewa kazi ya kuua adui kwa penalti. Hadi sasa ana mabao manane kwenye Ligi Kuu ambayo yanamfanya awe na jeuri.
Hata hivyo katika idadi hiyo ya mabao, matatu pekee ndio amefunga kawaida huku matano akitupia kwa penalti na hajakosa hata penalti moja msimu huu.
Alianza kutupia katika ushindi wa 2-1 mbele ya Mbao FC, akatupia katika kichapo cha 1-2 mbele ya Mwadui FC, akafunga kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Akatupia kwenye ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Lipuli FC na kisha akaizamisha Mtibwa Sugar kwenye ushindi wa bao 1-0.
Meddie Kagere (Simba) naye amefunga mabao manne kwa penalti akifunga kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya
Kagera Sugar, Simba 4-0 Mbeya City na katika sare ya 2-2 dhidi ya Yanga na kwenye ushindi wa bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar Uwanja wa Taifa.
Ukiachana na wakali hao, yupo pia Abdul Hillary (KMC) aliyefunga mabao matatu akifunga kwenye sare ya bao 1-1 mbele ya Yanga, vilevile kwenye kichapo cha 1-2 mbele ya Polisi Tanzania na pia walipolala kwa 2-3 mbele ya Polisi Tanzania katika mchezo wa mzunguko wa pili.
Yupo pia Sixtus Sabilo (Poisi Tanzania) aliyefunga kwenye sare ya bao 1-1 mbele ya Biashara United na waliposhinda mabao 2-1 mbele ya Kagera Sugar.
Wengine waliofunga kwa penalti ni David Kameta (Lipuli FC) wakitoka sare ya 2-2 na Tanzania Prisons,
Serge Alain wa KMC 2-1 Biashara, Awesu Awesu (Kagera Sugar waliposhinda  KMC 2-1 na Rajab Zahir wa Ruvu Shooting waliposhindwa na JKT 2-1.
Aggrey Morris (Azam FC) 2-2 JKT Tanzania, Marcel Kaheza (Polisi Tanzania) 2-1 KMC, Shaban Idd (Coastal Union) 1-0 Tanzania Prisons na Richard Djodi (Azama FC) 1-1 Mtibwa Sugar.
Wapo pia kina Ayoub Lyanga (Coastal Union) 1-1 JKT Tanzania, Datius Peter (Mbao) 1-1 Alliance, Danny Lyanga (JKT Tanzania) katika ushindi dhidi ya Mtibwa wa baoa 1-0, Seleman Ibrahim (Mbeya City) 2-1 Lipuli FC, Deogratias Munishi (Lipuli) walipofungwa na Mbeya City 2-1.