Juventus yamuweka Dybala sokoni kibabe

Muktasari:

Kwa sasa mchezaji huyo ambaye angekuwa na uhakika wa namba pale Old Trafford huenda akadondokea PSG ambako iwapo Neymar na Cavani hawataondoka anaweza kukumbana na mtihani mwingine wa kugombania namba kikosini ama kujikuta akisugua benchi.

Saa chache baada ya dili baada ya dili lake kutua Manchester United kugonga ukuta, nyota wa Juventus, Paulo Dybala amekutana na msala mzito klabuni, mara akitakiwa kuondoka majira haya ya kiangazi.

Kocha Mauzio Sarri amemtaka mshambuliaji huyo aliyegomea mshahara wa Pauni 180,000 alioahidiwa na Mashetani Wekundu aondoke klabuni kwa sababu hayupo kwenye mipango ya muda mfupi na mrefu ya kocha huyo na klabu kwa ujumla.

Kwa sasa mchezaji huyo ambaye angekuwa na uhakika wa namba pale Old Trafford huenda akadondokea PSG ambako iwapo Neymar na Cavani hawataondoka anaweza kukumbana na mtihani mwingine wa kugombania namba kikosini ama kujikuta akisugua benchi.

Tayari Kocha Sarri amekwishamtamkia hadharani kuwa hamhitaji ikiwa ni siku chache baada ya kuinasa saini ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Romelu Lukaku aliyetua klabni hapo kwa dau la Pauni 73 milioni.Mbali na Dyabala, pia Sarri amemtaka Mauro Icardi kuondokana klabuni.