Jose Mourinho aanza kumkumbuka Rooney

Kocha Jose Mourinho amesema kati ya vitu vilivyomuumiza ni kumuaga Wyne Rooney wakati akiondoka kwenda Everton baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 13.

Mourinho anasema, alijisikia uchungu alipomwambia mchezaji huyo kwa heri kabla ya kuondoka klabuni hapo na kwenda kujiunga na Everton.

Kocha huyo anaamini kwamba Manchester United itabaki kuwa nembo ya ubora kutokana na mabao aliyofunga na kuweka rekodi kabla ya kurudi kalbu yake ya zamani ambako kwa sasa anauhakika wa kucheza kikosi cha kwanza.