Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jogoo lampa mzuka Aucho

Muktasari:

  • Zawadi hiyo amepewa na shabiki wa Yanga, baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons wa ushindi wa mabao 2-1.

KIUNGO mkabaji wa Yanga, Khalid Aucho amesema jogoo aliyepewa na shabiki wa timu hiyo kutoka Mbeya, Peter Henry Chiwanga ana uwezo wa kumla peke yake.

Zawadi hiyo amepewa na shabiki wa Yanga, baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons wa ushindi wa mabao 2-1.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo ya kuku, Aucho amemshukuru shabiki huyo na kuahidi kuendeleza ubora wake kwa kuipambania timu kufikia malengo.

"Ni nadra sana kiungo kuonwa na kupewa zawadi, hili limenipa faraja kwani mara nyingi washambuliaji ndio wamekuwa wakipata fursa hizi za zawadi kutokana na kufunga;

"Nimefurahi kuipokea zawadi niliyopewa na kuhusu kumla na nani hii ni mipango yangu, lakini kwangu kula kuku mzima ni kawaida ni kutokana na namna ninavyofanya mazoezi," alisema.

Akizungumzia kiwango chake Aucho alisema anapenda kazi yake na amekuwa akifanya mazoezi mara kwa mara ili kujiweka fiti kwa lengo la kuona anafanya kilicho bora ndani ya Yanga.

"Nimeajiriwa kucheza na walinichukua kutokana na ubora niliokuwa nao, hivyo nitaendelea kupambana kuwa bora ili kuhakikisha nafanya kilicho bora," alisema.

Aucho alitoa pasi safi kwa Yao ambaye alimwaga maji kwa Pacome Zouzoua na kukwamisha mpira nyavuni akifunga bao la pili na la ushindi kwa Yanga.