Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKT yanasa saini ya kiungo Simba

Muktasari:

  • Simba ilikuwa kwenye mpango wa kumsainisha mkataba wa mwaka mmoja mchezaji huyo, wakati huohuo JKT Tanzania ilikuwa inahitaji huduma yake lakini wanajeshi wamefanikiwa na kumsainisha miaka miwili.

Zilikuwa ni fununu za kiungo Mshambuliaji wa SImba Hassan Dilunga kuhusishwa kwenye usajili wa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na JKT Tanzania

Simba ilikuwa kwenye mpango wa kumsainisha mkataba wa mwaka mmoja mchezaji huyo, wakati huohuo JKT Tanzania ilikuwa inahitaji huduma yake lakini wanajeshi wamefanikiwa na kumsainisha miaka miwili.

Kocha wa JKT, Malale Hamsini alishawahikuliambia Mwanaspoti kuwa anahitaji kusajili wachezaji wenye kiwango cha juu ambao wataonyesha ushindani, kwani hawataki yajirudie mambo ya miaka ya nyuma yaliyowashusha daraja.

"Ripoti niliyowapa viongozi ni kunisajilia wachezaji nafasi tatu ambazo ni  mshambuliaji, kiungo na beki ili kupata nguvu maeneo hayo ambayo yataongeza changamoto;

"Tunaingia kwenye ushindani mkubwa, tunahitaji kuwa bora kila eneo kuhusiana na Dilunga bado hatujamsainisha hilo naliacha kwa viongozi ni kweli tulikuwa naye kwenye mazoezi na nimemuona," alisema Malale.

Malele alisema wanatambua ugumu wa ligi hawatafanya makosa kwenye usajili lengo ni kuona timu hiyo hairudii makosa na kujikuta inarudi Championship tena.

Alisema wataongeza wachezaji wachache watakaoongeza ushindani kwa waliopo ambao waliipambania timu kuanzia chini na kuipandisha kwani wana uwezo mzuri ila wanahitaji kuongezewa nguvu