Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jamani mimi sio Maniche

Muktasari:

Mwanaspoti kupitia kona hii ya Mpaka Home iliamua kufunga kiguu na njia mpaka nyumbani kwa mchezaji huyo, ili kukata mzizi wa fitina.


KUFANANA jina na kiungo mshambuliaji wa Simba, Awadh Juma ‘Maniche’ kumekuwa kukiwachanganya mashabiki wa soka wakidhani Maniche amepelekwa kwa mkopo African Lyon. Ila ukweli Awadh Juma wa Lyon ni mchezaji mwingine kabisa na Maniche aliyetua Msimbazi enzi za utawala wa Ismail Aden Rage akitokea Mtibwa.

Mwanaspoti kupitia kona hii ya Mpaka Home iliamua kufunga kiguu na njia mpaka nyumbani kwa mchezaji huyo, ili kukata mzizi wa fitina.

Jamaa anaishi maeneo ya Mabibo Hosteli jijini Dar ambako anaishi na meneja wake aliyemtaja kwa jina la Oscar Milambo.

Awadh huyu anatokea Mtwara na sio Zanzibar kama ilivyo kwa Maniche wa Simba, lakini cha ajabu wote wanacheza nafasi moja yaani ya kiungo mshambuliaji.

Anafichua sababu ya kuishi na meneja wake hapa Dar es Salaam kwa vile ndiye kila kitu kwake baada ya kumhamisha kutoka kwao Mtwara kuja mjini ambako mpaka sasa mambyo yanamwendea vizuri.

Awadh ameweka bayana majina yake kamili ni Awadh Salum Mkana Juma na hilo, lilitambulika na kupata umaarufu zaidi alipokuwa Yanga B kwa sababu ya Maniche wa Simba ndio kisa cha kutumia jina la Awadh Juma. Si unajua vijana wanapenda kufanananisha.

 

NYUMBANI

Mwanaspoti: Hodi!

Awadh: Karibu. Hapa ndiyo nyumbani na naishi na meneja wangu ambaye ndiye amefanikisha kuishi hapa Dar es Salaam baada ya kuniibua kwenye michuano ya Umisseta, Kibaha.

Mwanaspoti: Kwa nini hujitegemei?

Awadh: Meneja hataki kabisa kusikia neno naondoka, anataka kuona maendeleo yangu hadi nafanikiwa nikiwa karibu naye, pia ana nyumba mbili hii na nyingine iko Mbezi hivyo wakati mwingine anakaa huko. Nitaanza kuishi maisha ya kujitegemea baadaye mambo yatakapokuwa mazuri zaidi.

Mwanaspoti: Unapokuwa nyumbani huwa unafanya nini?

Awadh: Nafanya kazi zote za hapa nyumbani ambapo kabla ya kwenda mazoezini asubuhi, huwa naamka saa 11, nafanya usafi nyumba yote kufagia, kupiga deki na mambo mengine ndiyo naondoka. Huwa napika pia na chakula ninachokipenda ni wali nyama, ingawa wakati mwingine ninarudi nimechoka huwa nanunua tu.

Si unaona namna nyumba ilivyo safi, kufagia, nafagi kweli na ninapokuwa nimemaliza shughuli zangu zote huwa natulia, nasikiliza muziki, naangalia televisheni au nalala tu.

 

MAPENZI

Mwanaspoti: Vipi unayemchumba?

Awadh: Mhuu! Mimi bado mdogo, sina mchumba bwana.

Mwanaspoti: Una miaka mingapi hata rafiki wa kile unayempenda pia huna?

Awadh: (Anacheka) Mbona maswali mengi, kweli ninaye rafiki wa kike na anaishi hapa hapa Dar es Salaam, anasoma Sekondari ya Makongo ni rafiki yangu wa stori tu na siyo mambo mengine.

Mwanaspoti: Kitu gani ulichompendea?

Awadh: Nimempenda kwa sababu ni mshauri mzuri. Huwa ananisaidia kwa ushauri katika mambo mengi mazuri ili nifanikiwe. Ni mzuri na mweupe.

 

HISTORIA KISOKA

Mwanaspoti: Historia yako kisoka iko vipi?

Awadh: Tulikuja kwenye Mashindano ya Umisseta, Kibaha. Wakati huo nilikuwa kidato cha pili Shule ya Sekondari Mkonge iliyopo Mtwara na ndipo meneja wangu Milambo aliponiona. Kwa sababu yeye ni mwalimu wa michezo Makongo alinichukua na kuanza kusoma Makongo hadi nilipomaliza kidato cha nne.

Lakini wakati nikiwa Makongo, Salvatory Edward alinichukua na kunisajili Yanga B ambayo niliichezea mwaka jana na baadaye alipoitwa African Lyon kwa sababu alikuwa anapenda kiwango changu, akanihamisha huko.

Nikasajiliwa na African Lyon mwaka jana na kucheza mechi za kuipandisha Ligi Kuu , lakini kwa bahati mbaya, Salva aliondoka na akaniacha hapa nikiichezea mpaka sasa.

Mwanaspoti: Nafasi gani unayopenda kuicheza?

Awadh: Ni kiungo mshambuliaji, ingawa nafasi zote za kiungo naweza. Winga na nyingine kulingana na mahitaji ya kocha wangu niwapo uwanjani.