Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya Aziz KI, Yanga ipo hivi

Muktasari:

  • Aziz KI aliyefunga bao moja na kuasisti mbili katika michuano hiyo ya CAF hatua ya makundi, amevunja ukimya alipozungumza na Mwanaspoti saa chache baada ya Yanga kukwama kutinga nusu fainali mbele ya Mamelodi baada ya kufungwa kwa penalti 3-2, huku bao lake likikataliwa dakika ya 59.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki amemaliza utata juu ya taarifa amegoma kusaini mkataba mpya na klabu hiyo na alikuwa mbioni kutua Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, akisema bado yupo yupo sana ndani ya kikosi hicho hadi atakapotwaa nao taji la Afrika.

Aziz KI aliyefunga bao moja na kuasisti mbili katika michuano hiyo ya CAF hatua ya makundi, amevunja ukimya alipozungumza na Mwanaspoti saa chache baada ya Yanga kukwama kutinga nusu fainali mbele ya Mamelodi baada ya kufungwa kwa penalti 3-2, huku bao lake likikataliwa dakika ya 59.

Nyota huyo kutoka Burkina Faso na anayeongoza kwa mabao Ligi Kuu Bara akifunga 13 sawa na Feisal Salum ‘Fei Toto; wa Azam, alisema ameshamalizana na Yanga na taarifa anaondoka ni uzushi unaopaswa kupuuzwa.

“Sina nia ya kuondoka hapa nimeletwa kwa sababu maalumu kama mpango huo hautokamilika nitaendelea kusalia kuitumikia timu ninayoipenda kwa moyo wangu wote, hata fedha haitaweza kujaza upendo nilionao kwa timu hii,” alisema Aziz KI na kuongeza;

“Rais Hersi Said alinisainisha hapa kwa sababu ana malengo ya kuona timu hii inatwaa mataji ya kimataifa hili sikuwashirikisha nitakuwa hapa kwa kufanya hayo, naomba mfahamu kwa nini aliniamini na kunileta hapa yeye pamoja na kamati yake.”

Aziz Ki alisema kwa matokeo iliyopata Yanga juzi yamemnyima usingizi na kukosa amani kabisa kwani alikuwa na ndoto za kuisaidia timu hiyo kuandika rekodi mpya ya kucheza nusu fainali, lakini amekwama na amelichukua kama funzo na yeye pamoja na timu watarudi upya na kwa nguvu msimu ujao.

“Nina deni kubwa na timu na nitapambana kwa kusaidiana na wenzangu tuweze kufikia malengo hasa kutwaa mataji ya kimataifa, Yanga ni maisha yangu. makubwa ambayo naweza kuyaeleza lakini ambayo yanapiga sana moyoni mwangu sisi sote ni familia ya Rais Hersi ambaye ninaweza kumuelezea kama baba na washiriki kadhaa,” alisema Aziz KI na kuongeza;

“Katika klabu hii lazima nipambane ili niwe katika kiwango cha klabu hii na inastahili kiwango cha juu na nitakaa hapa mpaka nifike huko ambao ninawiwa na nyinyi mashabiki wote kwa sababu mapenzi yenu kwangu hayana thamani kamwe ni makubwa sana.

“Natumai kupona kutoka kwa tamaa hii ya kibinafsi haraka iwezekanavyo na nipe yaliyo bora zaidi katika siku zijazo na tuonane mwaka ujao.”

Aziz Ki alijiunga na Yanga msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili na amebakiza miezi michache tu kuukamilisha, huku akifichua ataendelea kuwepo ndani ya kikosi cha Yanga kwa vile ameshamalizana na mabosi wake, japo alikataa kuweka bayana amesaini mkataba huo na kwa muda gani.